HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 6, 2023

MIUNDOMBINU KIPAUMBELE SERIKALI AWAMU YA SITA



Serikali imesema itaendelea kuhakikisha inawekeza kwenye miundombinu yote nchini ili kuwezesha sekta hiyo kukua kwa kasi huku ikichangia kwenye pato la taifa na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji jijini Arusha Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema uwekezaji huu haufanywi tuna Serikali bali unahusisha sekta binafsi na wadau wa maendeleo.

“Mkutano huu ni muhimu sana kwani sisi tunatekeleza miradi na kutunga Sera lakini ziko taasisi zinatekeleza miradi hiyo na wako wahisani wanaofadhili miradi hiyo hivyo tunapokutana kwa pamoja kila mmoja anatoa maoni ya mwenendo wa sekta ili kupata matokeo chanya’ amesema Waziri Prof Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ametumia Mkutano huo kuzitaka taasisi zote zinazosimia miradi ya maendeleo kuhakikisha zinasimamia kwa karibu miradi hiyo ili ikamilike kwa viwango na kwa wakati.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa Serikali imebadilisha sheria ya reli namba 17 ambapo imeruhusu sekta binafsi kuendesha reli ya kisasa ya SGR ili kupata tija ya uwekezaji mkubwa uliowekwa katika mradi huo.

Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya Joceline Cornet ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha katika miundombinu yote nchini lengo likiwa kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo inayokwenda ndani na nje ya Tanzania.

Cornet ameihakikishia Serikali kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Serikali ili kufikia malengo hususani katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu nchini.

Naye Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya viwanja vya ndege hususani kiwanja cha Arusha na kuiomba Serikali ikamilishe sehemu ya mradi wa kuweka taa ili kuwezesha uwanja huo kufanya kazi kwa saa 24.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wadau mbalimbali wa Uchukuzi wakati uzinduzi wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikabidhiwa tuzo ya Kutambua mchango wake kwenye Sekta ya  Uchukuzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara (kulia) wakati wa kufungua Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  Bw. Hamza Johari tuzo ya mshindi wa pili ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023 wakati uzinduzi wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akitoa tuzo   ya Mshindi wa pili ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023 kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw, Mussa Mbura  wakati uzinduzi wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Uchukuzi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari alipokuwa anaelezea kuhusu Mamlaka hiyo inavyokisimamia Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw, Mussa Mbura kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo kuhusu namna walivyojipanga kuweza kupunguza Ajali za Barabarani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad