HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 18, 2023

MILIONI 200 KUSAIDIA VIJANA KATI YA MIAKA 14-24

 Kaimu Mkuu wa Furahika Education College Tanzania, Dkt. David Msuya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Desemba 18, 2023.

Baadhi ya wanafunzi wakiangalia matokeo yao katika  chuo cha Furahika Education College Tanzania, kilivhopo Ilala Malapa jijini Dar es Salaam leo, Desemba 18, 2023.

CHUO cha Ufundi Stadi cha Furahika, kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam, kilichosajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVE) kimepokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwaajili ya kutekeleza mradi wa elimu bure kwa vijana.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Furahika Education College Tanzania, Dkt. David Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Desemba 18, 2023. Amesema kuwa katika kutekeleza mradi wa Vijana wa elimu Shirika la Furahika kupitia wizara ya elimu na Wizara ya maendeleo ya Jamii wanafanya ya kuwasaidia vijana kuondokana na utegeemezi kwa kuwapa elimu ya ufundi stadi ambapo wataweza kujikwamua katika maisha yao.

“Tumepokea shilingi milioni 200 kwaajili ya kusaidia vijana kwa mpango wa elimu bure ambao vijana hao wanapaswa kusajiliwa kuanzia sasa mpka Januari 20, 2024.”

 Dkt. Msuya ameishukuru Serikali kupitia wizara ya Elimu, Wizara ya Ustawi wa jamii kwa kutoa fedha ambazo ziatasaidia vijana ambao hawana uwezo wa kitanzania kupata elimu bure katika taasisi hiyo.

Amesema programu za Mradi huo zinawasajili hasa vijana waliopo tuu nyumbani ambao wamemaliza darasa la Saba hadi kidato cha nne kuanzia miaka 14 hadi miaka 24.

Amesema kituo hicho kinashirikiana na mashirika mbalimbali ili kuwasasidia vijana ambao hawakubahatika kupata elimu ya juu ili kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao katika jamii na nchi kwa ujumla.

“Tunafundisha hapa ili kila kijana ajifunze kwa vitendo, aweze kujiajiri mwenyewe, kumwongezea jitihada za kuwasaidia vijana wezake ili wakawe baraka kwa watu wengine kwa maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.” Amesema Dkt. Msuya

Amesema mafunzo hayo wanayoyatoa yatamwezesha kijana mafunzo ambayo yatamwezesha kuaminika machoni kwa waajiri au kwenye viwanda mbalimbali.

Pia taasisi ya furahika inaungana na Serikali kupinga ukatili wa jinsia ambao unafanyika katika jamii ambapo ameiomba Serikali kuandaa mpango kwaajili ya mtu yeyote au jamii anayemtuma mtoto kufanya biashara muda wa masomo kuchukuliwa hatua dhidi ya kitendo cha kumnyima mtoto haki ya kupata elimu katika taifa.

“Watoto wengi wanatumwa kufanya biashara muda wa masomo, na wale wanaowasafirisha kutoka vijijini kuwaleta hapa Dar es Salaam ili wawatumikishe kwenye kazi za ndani wachukuliwe hatua kwani jambo hilo si jambo jema.” Ameongeza Dkt. Msuya

Amesema maisha ya unyanyasaji ndio yanayoongeza wimbi la unzinzi kwa watoto wa miaka 15 hadi 18.

“Jambo hili kimaadili ya taifa letu tunalikemea kulingana na wiki ya kupinga ukatili, halikubaliki na tunaiunga mkono Serikali na mkuu wa mkoa ili aweze kuendelea kuchukua hatua ya kuvunja vijiwe vilivyowekwa kwaajili ya wadada wanaofanyabiashara ya ngono kwani vitendo hivyo vinaleta maadili mabaya katika nchi yetu.”

Pia amesisitiza kuwa mtoto asome ili awe na kitu cha kufanya asijiingize katika makundi mabaya na kama mtoto ameshindikana apelekwe katika kituo hicho ili ajifunze kushona, usindikaji wa kahawa, ajifunze masuala ya utalii, kwani yanatolewa bila gharama yeyote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad