Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata, akimkabidhi tuzo ya ushindi wa mauzo ya nje ya Mgodi wa North Mara, kwa Meneja wa Kodi wa Barrick, Judith Chambua, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, (kulia) ni Mtaalamu wa masuala la kodi wa Barrick (Tax Specialist), Amos Milanzi.
Tuzo
---
Ubia wa kampuni ya Barrick Gold Corporation na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation. unazidi kuleta mafanikio ambapo mgodi wake wa Barrick North Mara, umetunukiwa tuzo ya kulipa kodi ya mauzo ya nje (Substantial Taxes and Duties for exported Goods).
Tuzo hiyo ya kutambua mchango wa Mgodi wa Barrick North Mara, ilitolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakati wa maadhomisho ya Wiki ya shukrani kwa Mlipa Kodi yanayoandaliwa na Mamlaka hiyo.
Mgodi huo ambao unaendelea kuleta mabadiliko chanya kutokana na kufanikisha miradi mbalimbali ya kijamii mkoani Mara kupitia fedha za Uwajibikaji kwa jamii (CSR),pia umefanikiwa kuanzisha mradi wa Biashara Kilimo kwa lengo la kuwapatia vijana wanaotoka maeneo yanayozunguka mgodi ajira kupitia kilimo pia wanafundishwa mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa na kuhakikishiwa soko la uhakika wa mazao wanayozalisha.
Katika Kipindi cha mwaka jana mgodi wa Barrick North Mara uliongoza kwa kulipa kodi nchini na kutunukiwa tuzo ya Mlipa kodi Bora.
No comments:
Post a Comment