*Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu wahimizwa kutumia fursa hiyo
Na; Mwandishi Wetu – Bujumbura, BURUNDI


Mhandisi Luhemeja amesema kuwa maonesho hayo yamewezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kutambulika kimataifa huku ameshukuru
Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha wajasiriamali 259 kwenda Burundi kutangaza bidhaa na huduma zao.
Aidha, Katibu Mkuu huyo amewahimiza Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu kutumia fursa ya maonesho hayo kujiajiri na kuondokana na umaskini.
Naye, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa amewahamasisha wajasiriamali kutumia fursa ya maonesho hayo ili kutangaza bidhaa za Tanzania, kukuza ujuzi na masoko ya bidhaa zao pamoja na kukuza teknolojia ya utengenezaji wa bidhaa.
No comments:
Post a Comment