HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 17, 2023

KAMPUNI YA iStore WATOA MAFUNZO KWA WATEJA WAKE

 KAMPUNI ya iStore kupitia chapa ya simu aina ya iPhone wamefanya mazungumzo wadau wake juu ya bidhaa mpya ambazo wamezianzisha na hafla ya kuuaga mwaka 2023 katika hoteli ya Slipway Masaki Jijini Dar es Salaam, hafla iliyofanyika mwishoni mwa  wiki.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa semina fupi iliyoshirikisha wateja na watumiaji wa simu aina ya iPhone Mkurugenzi wa Kampuni ya iStore nchini Tanzania,  Vipul Shaah amesema kukutana na wateja wao ni sehemu moja ya kufikisha elimu mbalimbali juu ya matumizi za simu za iPhone pamoja na kutambulisha bidhaa mpya zinazoingia sokoni.

"Nafasi hii ya kukutana na wateja wetu ni kuwapatia elimu jinsi gani wanaweza kutumia simu za iPhone pamoja na iPad ambazo mara nyingi zimekuwa zikileta mfumo mpya wa matumizi wa vifaa hivi, hivyo kukutana kwetu ni nafasi pekee mteja kufanya chaguo la bidhaa bora bila kuwepo kwa kizuizi cha kutofahamu  kutumia programu au mfumo uliopo kwenye kifaa hicho."

Aidha Shaah ameongeza pia amesema wamezindua programu mpya itakayopatikana katika imac ambayo itakayopatikana kwa rangi 7 za kumvutia mteja.

Pia amesema matarajio yao makubwa kwa Wateja wao kueneza uelewa huo juu ya mifumo na programu zinazopatikana katika iMac na wapo tayari kuwapa bidhaa zilizo bora zaidi

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya iStore Karigo amesema kuwa moja kati ya bidhaa hizo iPhone kwaajili ya mtanzania,

Pia amesema kuwa kampuni hiyo inamsadia mteja kuweza kubadilisha i Phone aliyonayo kwa kulingana na toleo ili kupata toleo jipya na la kisasa.

Akizungumzia kuhusiana na gharama amesema kuwa gharama za iPhone zao ni rahisi kabisa na ni iPhone ambazo ni toleo halisi (Original) kulingana na nchi ambapo zinatoka.

Ameongeza kuwa kwa wale waonunua simu katika kampuni yao wanauwezo wa kuipeleka simu kwaajili ya matengenezo pale inapoharibika ndani ya miaka miwili tangu kuinunua bila gharama yeyote.

Mkurugenzi wa Kampuni ya iStore nchini Tanzania,  Vipul Shaah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama mara baada ya kutoa elimu kwa wateja wake.
Afisa Masoko wa Kampuni ya iStore Karigo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama mara baada ya kutoa elimu kwa wateja wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad