HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 1, 2023

NBAA YATOA MILIONI 15 HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI KWA AJILI YA WATOTO WENYE SARATANI

 Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa hundi yenye thamani Shilingi Milioni 15 kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaogua Saratani wanaopatiwa matibabu hispitalini hapo.


Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno amesema leo tumekuja hapa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ambapo tuna kongamano letu linalofanyika kila mwaka na tumekuwa tunafanya mambo mengi ikiwa ni kurudisha kwa jamii ambapo mwaka huu tumeamua kwa tusaidie kidogo kwa kuonesha mfano kwa watoto wanaoangaika na Saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuweza kuchangia.

Maneno amewasisitiza wadau kushiriki katika kutoa msaada kwa wagonjwa ikiwa ni hali ya kurudisha kwa jamii ambapo leo Bodi ya NBAA imeamua kuja kuoa msaada wa Waasibu na Wakaguzi wa Hesabu walioutoa ikiwa ni kurudisha kwa jamii ili kuweza kukuza huduma za kijamii.

Pia amewashukuru wafanyakazi wote wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa kuendelea kutoa huduma pamoja na kuendelea kufanya maboresho katika hospitali hiyo ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea hasa kwenye Afya kwa kuwa na vifaa bora.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi meishukuru Bodi ya NBAA kwa kuweza kuwatanisha Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kuja na wazo la kusaidia watoto wenye magonjwa wa Kansa wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amewaomba wadau wengine kuweza kuwasaidia watoto hao pamoja na wangonjwa mbalimbali katika Hospitali hiyo.

“Matibabu ni ghali lakini tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwakuweza kuja nawazo la Bima ya Afya kwa wote ambapo mpaka sasa Bunge limeweza kupitisha Sera hiyo ambapo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwenye suala zima la Matibabu.” Alisema Dkt. Magandi.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno akimkabidi hundi ya shilingi Milioni 15 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi kwa ajili ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni moja ya Maadhimisho ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, CPA Ashraph Yusuph  akionesha hundi  ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni moja ya Maadhimisho ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Redempta Matindi, Wa kwanza kulia ni  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno akizungumza kuhusu mchango wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu walivyoamua kurudisha kwa jamii kwa kukabidhi msaada wa Milioni 15 kwa ajili ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni moja ya Maadhimisho ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi akiwakaribisha wageni pamoja na kuzungumzia hali ya Matibabu katika Hopitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Mloganzira wakati wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada Watoto wenye ugonjwa wa Saratani ikiwa ni kurudisha kwa jamii.
Baadhi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, Madakatar na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wafanyakazi wa  Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya NBAA CPA ,Pius Maneno wakati wa kutoa msaada  kwa ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, CPA Ashraph Yusuph akitoa neon la Shukrani kwa uongozi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa kushirikiana na Wahasibu na Wakaguzi kutoa mchango kwa ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meza kuu (waliokaa) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno (katikati waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi (wa tatu kushoto waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na madakatari pamoja na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kutoa msaada  kwa ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meza kuu (waliokaa) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno (katikati waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi (wa tatu kushoto waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya NBAA waliofika kwa ajili ya kutoa msaada  kwa ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meza kuu ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA ,Pius Maneno (katikati waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi (wa tatu kushoto waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu waliofika kwa ajili ya kutoa msaada  kwa ya Watoto wenye ugonjwa wa Saratani wanaotibiwa katikaHospitali ya Taifa ya Muhimbili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad