HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 18, 2023

GF KIBAHA WAPEWA TUZO YA MUUNGANISHAJI BORA WA MWAKA


KAMPUNI ya Unganishaji wa Magari nchini Tanzania GF Vehicle Assembler iliyopo Kibaha Pwani, leo imeweza kuibuka kinara katika Tuzo ya Muunganishaji bora wa wa magari wa mwaka kwenye usiku wa Tuzo za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Tuzo hizo zinaumuhimu hutolewa kwa mwaka mara moja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuratibiwa na shirikisho la Viwanda nchini CTi.

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amemkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Biashara na Masoko GF Truck, Salman Karmal.

Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo, Salman Karmal amesema Tuzo hiyo inawapa nguvu ya kuendelea kuzalisha (Kuunganisha Magari) kwa ubora na kuongeza uzalishaji.

"Kwa mwaka 2023 tumeweza Kuzalisha gari 2000 na mategemeo yetu ni kuzalisha zaidi kwa mwaka 2024 kufikia gari 3500 kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya soko." amesema Karmal.

Amemaliza kwa kusema GF inaendelea kuishika mkono Serikali katika sera ya wazalishaji wa ndani (local Content).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad