HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 10, 2023

FAINALI ZA MICHUANO YA CHAMWANA SUPER CUP ZATAMATIKA MAGUNIA

Diwani wa Kata ya Kinondoni Idrisa Said Ngatiche akizungumza na Wanahabari mara baada ya Kumalizika Fainali ya michuano ya Chamwana Super Cup yaliyofanyika katika Viwanja vya Magunia Msasani Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kata ya Msasani Hemed Chamwana akiongea machache namna walivyojipanga kwa mwaka 2024 katika Michuano ya Chamwana Super Cup huku akisisitiza zaidi Lengo la michuano hiyo ni kuwakitanisha pamoja Vijana kushiriki michezo.
Afisa Habari wa Kampuni ya Ubashiri (BETIKA) Juvenalius Rugambwa akiongea machache namna kampuni hiyo inavyoendelea kutoa sapoti katika michezo ya ngazi zote kwa mwaka 2023 na wataendelea kwa miaka ijayo kusapoti michezo.
*Betika Wamwaga vifaa vya Michezo

Na Khadija Seif , Michuzi TV
KATIKA Kuadhimisha kumbukizi ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Viongozi wa Serikali ya mtaa ya Msasani wameadhimisha siku hiyo katika kimichezo.

Akizungumza na Michuziblog Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Hemed Chamwana amesema michezo inakutanisha watu wengi hususani Vijana kutoka sehemu tofauti lengo ni kuimarisha Afya zao pamoja na kupata ajira za muda mfupi.

"Lengo la kuanzisha michuano hii ni kuwatengenezea mazingira vijana kukosa muda wa kufanya uhalifu na vitendo viovu badala yake muda huo utumike katika michezo."

Aidha amesema michuano hiyo itakuwa endelevu kwa miaka ijayo ili kuendelea kutoa hamasa katika michezo na kuzalisha vipaji vipya vingi.

Kwa upande wa Mgeni mualikwa wa fainali hizo Diwani kata ya Kinondoni Idrisa Said Ngatiche wakati wa Fainali za Chamwana Super Cup 2023 amesema amekuwa mdau mkubwa wa michezo na ataendelea kutoa ushirikiano huo kwa vijana kuhakikisha michezo ina imarisha Afya na inakuwa sehemu ya Ajira kwao.

"Wote tunatambua waasisi wetu wamepamba kupigania uhuru wetu ambao Leo sisi kama viongozi tunajivunia na tumeamua kuenzi uhuru huu kwa njia ya michezo,Leo tuna tamatisha fainali hizi katika Uwanja wa Magunia Kata ya Msasani."

Hata hivyo amewapongeza Waandaaji wa Chamwana Cup kwa kuunganisha vijana kwa pamoja kuhakikisha wanashiriki michezo kikamilifu.

Nae Kwa upande wake mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo Afisa Habari wa Betika Juvenalius Rugambwa amesema kuwa Kama Kampuni hiyo wataendelea kutoa hamasa katika michezo hasa kwa Chupukizi na kwa Mwaka 2023 umekuwa mwaka mzuri kwao kutokana na Kampuni kujikita zaidi katika michezo na kuwapa fursa wanabetika kushuhudia Fainali mbalimbali mubashara.

Aidha Mshindi wa kwanza katika fainali hizo ilikuwa timu ya Mgundini fc ambao wameibuka na kitita cha shilingi Milioni 1 wakati mshindi wa pili timu ya Beira fc akiibuka na seti nzima ya vifaa vya michezo ikiwemo jezi pamoja na mipira.

"Tuliunga mkono michuano hii toka awali na kwa tuliamua kumuunga mkono Mwenyekiti Chamwana kutokana tunajua michezo inawaleta karibu jamii yake na sisi kama Kampuni ya Betika Hatutaacha kushika mkono jamii katika michezo."

Pia Rugambwa ametoa wito kwa taasisi na makampuni mengine yaweze kusapoti michezo kwa ngazi zote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad