HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 28, 2023

Washiriki kutoka Tanzania na Eswatini wamaliza kozi ya ICAO ya wakaguzi wa usalama wa usafiri wa anga inayotolewa CATC kwa ufaulu wa juu


Jumla ya Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini waliokuwa wanahudhuria kozi maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)wamemaliza kozi hiyo ya siku saba kwa ufaulu wa juu.

Akifunga kozi hiyo Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje amewapongeza washiriki wa kozi hiyo kwa juhudi zao zilizowawezesha darasa zima kupata vyeti vya kumaliza badala ya vyeti cha kushiriki.

Kanje aliongeza kuwa chuo cha CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

Kozi hiyo ya ICAO imeendeshwa na watanzania waliothibitishwa na ICAO, Christine Bgoya kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA)na Daniel Makina Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).

Kozi hiyo iliyoanza Novemba 20, 2023 imemalizika Novemba 28, 2023 na imehudhuriwa na jumla ya washiriki 21 kutoka CATC, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juluius Nyerere (JNIA)na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA), Mashirika ya kutoa huduma za ndege ya NAS (DAR&KIA), United Aviation, Shirika la ndege la Precision na Mamlaka ya Usafiri wa Usafiri wa Eswatini (ECAA).
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini mara baada ya kufunga kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akizungumza wakati wa kufunga kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa Anga kwa Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini iliyofanyika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mratibu wa Mafunzo ya ASTC katika Chuo cha CATC, Neema Msumi akitoa mrejesho wa mafunzo ya kozi hiyo kwa Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje wakati wa kufunga kozi ya Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini waliohudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa Usafiri wa Anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkufunzi aliyedhibitishwa na ICAO  kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Christine Bgoya (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakufunzi kwa Chuo cha CATC wakati wa kufunga kozi ya Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akikabidhi vyeti vya kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa Usafiri wa Anga kwa Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini waliohudhuria kozi hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria Kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa kufunga kozi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad