HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 20, 2023

Washiriki kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya ICAO ya wakaguzi wa usalama wa usafiri wa anga inayotolewa CATC

 

Jumla ya Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Akifungua kozi hiyo Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje amewakaribisha washiriki hao chuoni hapo na kuwataka kuhakikisha wanapomaliza masomo yao wanaondoka na cheti cha kumaliza badala ya cheti cha kushiriki.

Kanje aliongeza kuwa chuo cha CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

Kozi hiyo ya ICAO inaendeshwa na watanzania waliothibitishwa na ICAO, Christine Bgoya kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) na Daniel Makina kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).

Kozi hiyo iliyoanza Novemba 20, 2023 itamalizika Novemba 28,2023 na inahudhuriwa na jumla ya washiriki 21 kutoka CATC, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juluius Nyerere (JNIA)na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar (ZAA), Mashirika ya kutoa huduma za ndege ya NAS (DAR&KIA), United Aviation, Shirika la ndege la Precision na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Eswatini (ECAA) .
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akizungumza na Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mratibu wa Mafunzo ya ASTC katika Chuo cha CATC, Neema Msumi akitoa ufafanuzi kuhusu kozi hiyo kwa Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje wakati wa kufungua kozi ya Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Mkufunzi aliyedhibitishwa na ICAO Christine Bgoya kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kozi ya Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
 Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguziwa kozi hiyo.
Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakaguzi 21 kutoka Tanzania na Eswatini wanahudhuria kozi ya maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad