MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetumia Sh. milioni 50 kujenga madarasa na kununua madawati, ikiwa ni shukrani ya mamlaka hiyo kwa walipakodi.
Akizungumza leo Novemba 22, 2023 alipokuwa akikabidhi madarasa na madawati hayo katika Shule ya Msingi Kisarawe II iliyopo Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna Mkuu wa Idara ya walipakodi wakubwa, Eunice Luheluka, amesema TRA imejenga madarasa mawili pamoja na madawati 100.
Amesema lengo ni kushiriki kwa namna ya pekee kugusa huduma za kijamii kwa wananchi kwa kuunga mkono juhudi za serikali kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Upendo Mahalu, ameishukuru TRA kwa ufadhili huo na kuyaomba mashirika na makampuni mengine kujitokeza kusaidia ujenzi wa miundombinu ya shule.
"Kama mnavyofahamu Wilaya yetu bado ni changa ina mahitaji mengi. Tuna upungufu wa madarasa na madawati japokuwa tumepata fedha kupitia mradi wa Boost, bado mahitaji ni makubwa," amesema.
Mkuu wa Shule ya Msingi Kisarawe II, Joseph Kavishe, amesema baada ya ufadhili wa TRA, shule inaupungufu wa madarasa 18 na madawati 192.
"Mradi huo utatusaidia kupunguza mrundikano darasani na utawawezesha wanafunzi 300 waliokuwa wanakaa chini kupata madawati. Tumeamua madarasa haya mapya yatumiwe na wanafunzi wa darasa la kwanza ili kuwapa utulivu wawapo shuleni," amesema.
Wednesday, November 22, 2023
Home
Unlabelled
TRA YATUMIA TH.50 MILIONI KUJENGA MADARASA NA KUNUNUA MADAWATI SHULE YA MSINGI KISARAWE II
TRA YATUMIA TH.50 MILIONI KUJENGA MADARASA NA KUNUNUA MADAWATI SHULE YA MSINGI KISARAWE II
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment