HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 1, 2023

SERIKALI YATOA TRILIONI 6.7 KUONGEZA UWEKEZAJI KATIKA TAFITI ZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 

Mkurugenzi wa huduma za Tiba kutoka wizara ya Afya, Prof. Paschal Rugajo akipokea Tuzo ya shukrani kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya, Muhimbili(MUHAS) Prof Apolinary Kamuhabwa (kushoto) wakati wa mkutano wa kimataifa wa kisayansi wa magonjwa yasiyoya kuambukiza uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Na Karama Kenyunko Michuzi tv
WAZIRI Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema serikali imetoa Sh trilioni 6.7 kwa ajili ya kuongeza uwekezaji katika utafiti, teknolojia, na miundombinu ya huduma za afya kwa lengo la kuimarisha hatua za kuzuia magonjwa yasiyoambukiza na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania wote.

Aidha, ameelekeza sekta ya afya nchini kuhakikisha inadhibiti gharama za kuzuia, kukinga na zile za matibabu kwa magonjwa yasiyoambukiza ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kuweza kutambua hali zao na kufuatiliwa kimatibabu.

Pia ameitaka Wizara ya Afya iendelee kushirikiana na sekta nyingine, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi ili kuhakikisha huduma hizo za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ynawafikia wananchi katika jamii zao.

Akifungua kongamano la kisayansi la magonjwa yasiyoambukiza leo Dar es Salaam, kwa niaba ya Waziri Majaliwa, Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya, Profesa Pascal Rugajo amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa tishio kubwa kwa afya na ustawi wa kwani yanawaathiri kimya kimya wananchi na, kudhoofisha maendeleo.

Amesema athari za magonjwa hayo ni zaidi ya mateso ya mtu binafsi kwani yanaathiri jamii, uchumi na mustakabali wa taifa.

Majaliwa amesema asilimia 67 ya magonjwa hayo yanatokea kabla ya umri wa miaka 40 na kwamba mbali na kuwa chanzo kikuu cha vifo duniani, magonjwa hayo pia yana gharama kubwa ambayo inaathiri siyo tu afya yanawasukuma watu katika ufukara, yanapunguza ufanisi kazini, na yanatishia ustawi wa kiuchumi, hususan katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Ameeleza kuwa kongamano hilo limewakutanisha wanasayansi, watafiti, wataalamu wa tiba, watunga sera na watu wenye uzoefu ikiwemo wale wanaoishi na magonjwa hayo kutoka maeneo mbalimbali kutoa ujuzi wao, kujadili mikakati mipya, na kutoa suluhisho za ubunifu kwa ufanisi wa kupambana na magonjwa hayo.

"Katika mikakati hiyo suala la utambuzi wa mapema, kuwekeza katika afya ya msingi hususani kupitia watoa huduma kwenye ngazi za jamii pamoja na kuhusisha jamii yenyewe katika kuzuia na kudhibiti magonjwa haya kumepewa kipaumbele cha juu. Jukumu letu sote ni kukumbuka kusimamia utekelezaji wa maelekezo haya," amesema.

Majaliwa amesema watajitahidi kuongeza ufahamu miongoni mwa wananchi kuhusu visababishi, vichochezi na viashiria vya hatari na umuhimu wa ugunduzi na ufuatiliaji wa mapema wa magonjwa haya kwa wakati.

"Lengo namba 3.4 la malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG) linazitaka nchi zote wanachama kupunguza vifo vya mapema kutokana na magonjwa yasiyoambukizwa kwa theluthi moja ifikapo mwaka 2030 kupitia kuzuia na matibabu; na kukuza afya ya akili na ustawi. Licha ya juhudi zilizofanywa, nchi nyingi zenye kipato cha chini na cha kati ziko nje ya shabaha ya kufikia lengo la SDG 3.4," amesisitiza.

Pia amesema NCDs inasababisha vifo milioni 41 kila mwaka, sawa na asilimia 71 ya vifo vyote duniani hususan katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati chini ya Jangwa la Sahara ambazo kwa sasa zinakabiliana na mzigo maradufu wa magonjwa na mifumo duni ya afya.

"Tanzania, kwa mwaka huu 2023, tunafanya utafiti wetu wa pili wa STEPs, utafiti wa kwanza uliofanyika mwaka 2012 ulionyesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la juu la damu ambapo asilimia 25.9 mtu mmoja kati ya kila watu wanne ana ugonjwa huo," ameeleza.

Vile vile, ameongeza kuwa mtu mmoja kati ya watu 10 sawa na asilimia 9.1 ana kisukari.

utafiti huo ulionesha uwepo wa ongezeko la tabia hatarishi kama matumizi ya tumbaku (15.9%n1 kati ya kila watu 6), matumizi makubwa ya pombe (29.3% 1 kati ya kila watu 3) na kutozingatia ulaji unaofaa ambapo ni asilimia 3% tu ya Watanzania waliokiri kula matunda na mboga kama inavyopendekezwa.

Hata hivyo, maeneo mengine yalioonekana kuwa na changamoto ni pamoja na uwepo wa viwango vya juu vya lehemu (26%-1 kati ya kila watu 4), na uzito mkubwa na unene (26%-1 kati ya kila watu 4).


Mkurugenzi wa huduma za Tiba kutoka wizara ya Afya, Prof. Paschal Rugajo akizungumza wakati wa mkutano wa Kimataifa wa Kisayansi wa magonjwa yasiyoya kuambukiza uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo Novemba Mosi, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya, Muhimbili(MUHAS) Prof Apolinary Kamuhabwa (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa kisayansi wa magonjwa yasiyoya kuambukiza uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba Mosi, 2023

Sehemu ya watafiti na wadau mbali mbali wa sekta ya Afya wakiwa wamesimama kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Prof. Paschal Rugajo aliyemuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano wa Kimataifa wa Kisayansi wa magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad