HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 25, 2023

PROF. NDALICHAKO AHIMIZA WAAJIRI KUZINGATIA KUAJIRI 3% YA WATU WENYE ULEMAVU.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewahimiza waajiri nchini kuendelea kutoa kipaumbele cha ajira kwa watu wenye ulemavu wakiwamo wasioona kwa mujibu wa sheria.
Na Mwandishi Wetu; Njombe.

Mhe. Prof. Ndalichako akizungumza Novemba 24, 2023 kwenye maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe kitaifa iliyofanyika mkoani Njombe, amesema "Kama Waziri mwenye dhamana na Watu wenye Ulemavu na kwa niaba ya Serikali napenda kuwahakikishia kwamba tutaendelea kusimamia kikamilifu suala la upatikanaji wa ajira kwa Watu Wenye Ulemavu kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 inayomtaka kila mwajiri anayeajiri kuanzia watu 20 kuhakikisha asilimia tatu ya waajiriwa wake ni Watu wenye Ulemavu.”

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka ametoa rai kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum mkoani humo kuhakikisha wanapelekwa shule.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema ofisi hiyo imefanikiwa kutengeneza mfumo wa kielektroniki wa taarifa na kanzi-data kwa watu wenye ulemavu.

Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLD), Omari Mpondelwa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu kwa kuwapatia vifaa wezeshi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza Wakati wa maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe kitaifa yaliyofanyika tarehe 24 Novemba, 2023 mkiani Njombe.

Baadhi ya Watu Wenye Ulevu wasioona wakifanya maandamano ya kutembea kwa lengo la kuadhimisha siku ya fimbo nyeupe kitaifa mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad