Akiwa amezaliwa na kukulia kijijini ambapo uchumi unategemea mashamba kwa kiasi kikubwa, Abdulmajid Nsekela ana shauku ya asili katika kilimo.
Nsekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, alizaliwa katika kijiji cha Nyakatuntu, wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.
Kumbukumbu zake za utotoni na ujanani zimejaa taswira ya shambani nah ii ndiyo chanzo cha shauku yake ya kukuza sekta ya kilimo Tanzania.
Safari yake kutoka shambani Nyakatuntu hadi kuongoza moja ya benki kubwa Tanzania, CRDB, imempa uelewa wa kutosha kuhusu changamoto za wakulima wadogo nchini. Uhusiano wake binafsi na kilimo umemfanya awe na nia ya dhati kuwainua wakulima wadogo na kuhakikisha sekta hiyo inakua kwa ujumla.
“Kukulia shamba kumenifanya nipende kilimo kwa dhati na ninajua ugumu wanaopitia wakulima. Kilimo siyo tu sekta ya uchumi bali ni njia halisi ya maisha na uhusiano huu ndiyo unaongoza dira yetu benki ya CRDB. Sisi ni washirika wa dhati katika maendeleo ya wakulima tukiwapa fursa za kutimiza malengo yao,” Nsekela alisema.
Akiongea katika mkutano uliohusu upatikanaji fedha kwa ajili ya kilimo hivi karibuni, Nsekela alidhihirisha dira yake katika kukuza kilimo kwa kuhakikisha upatikanaji wa fedha na pembejeo kwa wakulima.
Ili kufikia azma hiyo, alisisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi.
"Ili tujenge sekta ya kilimo imara, ushirikiano ni muhimu sana. Tunahitaji kuunganisha serikali, wafanyabiashara na jamii ili kuwakwamua wakulima na kulihakikishia Taifa chakula. Ni juhudi za pamoja.”
Karibu 43% ya fedha zinazoenda kwenye sekta ya kilimo zinatoka Benki ya CRDB. Benki hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na seikali ili kuwapatia wakulima fedha, mbolea na pembejeo zingine.
Benki hiyo pia inafanya kazi na wasambazaji ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo muhimu kwa uhakika.
Ili kuwafikia wakulima, Benki ya CRDB inashrikiana na vyama vya msingi vya wakulima (AMCOS) na vyama vya ushirika. Mojawapo ya matokeo ya ushirikiano huu ni mfumo wa stakabadhi ghalani ambao unawahakikishia wakulima kupata fedha kutokana na mazao yao.
Ushuhuda wa dhamira ya Benki ya CRDB ni kiasi cha mikopo iliyotolewa kwenye sekta ya kilimo ambayo inafikia TZS 801 bilioni (USD 334 milioni), na kuifanya benki kuwa ya kwanza nchini. Mikopo hiyo inajumuisha wasambazaji wa pembejeo, wachakataji wa mazao ya kilimo, na wafanya biashara ya kilimo.
"Kiasi hicho ni ushahidi tosha kuhusu dhamira yetu kwenye kilimo. Tunawekeza kwenye mnyororo mzima wa kilimo ili kuhakikisha mstakabali imara. Kupitia ushirikiano, tumetengeneza njia nzuri za wakulima kupata huduma zetu za kifedha pale wanapohitaji. Tupo nao wakati wa shida na raha,” alisema.
Nsekela alitaja moja ya huduma zinazowagusa wakulima ni akaunti ya FahariKilimo ambayo inawawezesha zaidi ya wakulima 50,000 ambao wananufaika na mikopo, bima ya afya kupitia Shirika la Bima la Taifa (NHIF). CRDB pia inatoa huduma za kibenki kwa wakulima kupitia AMCOS au wakala binafsi, na CRDB Wakalas, ambayo inatoa fursa za kuongeza kipato.
Benki ya CRDB mpango wa kuendeleza teknolojia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (TACADTP) mwaka huu na kuifanya iwe benki ya kwanza kupata idhibati ya Mfuko wa Kijani wa Umoja wa Mataifa (GCF).
Mpango huo umetenga USD 200 milioni kwa jili ya mikopo ya shughuli za kilimo ambazo zinahimili mabadiliko ya tabia nchi, kwa lengo la kuwawezesha watu 1.2 milioni moja kwa moja na wengine 4.9 milioni kupitia kwao.
"Kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi sio hiari bali lazima. Kupitia TACADTP, tunapanda mbegu ya uhimilivu na huku tukiwanufaisha mamilioni ya watanzania,” alisema.
Nsekela alisema shirika la kujitolea la benki hiyo (CRDB Bank Foundation) linafanya kazi nzuri kuwasaidia wakulima. Shirika hilo hutoa mafunzo na kutoa fedha kwa ajili ya wajasiriamali wadogo kupitia mipango yake kama vile IMBEJU. Jumla ya TZS 5 bilioni zimetengwa kusaidia wajasiriamali wadogo katika sekta mbalimbali ikiwepmo kilimo.
"Tunajivunia kuwawezesha watu wa chini kabisa. Shirika la CRDB Bank Foundation linahakikisha wajasiriamali wadogo wanakua na kuchangia katika kulijenga taifa,” alisema.
Nsekela pia alionyesha matumaini kwenye kilimo cha kidigitali nan a ushirikiano unaoendelea na taasisi za serikali, taasisi zinazotoa pamoja na wadau wengine kwenye mnyororo wa thamani katika kilimo
No comments:
Post a Comment