HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 3, 2023

MICHUANO YA DKT.SAMIA CUP YAZINDULIWA WILAYANI SAME

 Na Ashrack Miraji, Kilimanjaro


MKUU wa Wilaya ya Same Kaslida Mgeni amewaasa vijana kuacha tamaa kuiga tamaduni zisizo faa zilizo kinyume na maadili yaliyo kwenye jamii ikiwemo mchezo mchafu wa kujihusisha katika mapenzi ya Jinsia Moja (Ushoga na Usagaji).

Pia ameitaka jamii kutojihusisha na biashara haramu ya Dawa za Kulevya Kilimo cha Bhangi na mirungi kwani ni miongoni mwa viashiria vinavyotajwa kuathiri vijana kuwa katika hatari ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya Dkt.Samia Cup, mashindano yaliyo andaliwa na Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango akisema uamuzi huo wa Mbunge kuanzisha mashindano utasaidia kuibua vipaji hasa kwa vijana washiriki, pia kuimarisha afya kama inavyo sisitizwa na serikali miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na magonjwa nyemelezi.

“Kipekee nimshukuru Mbuge sote tunaona kazi kubwa anayoifanya kupambania wananchi kwenye jimbo lake hususani katika kuleta maendeleo hivyo niendelee kutoa rahi kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye michezo hii, kwakua itasaidia kupunguza muda wa kukaa vijiweni bila shughuli maalum ambako ndiko mnakutana na vishawishi na kujiingiza kwenye michezo isiyo faa, "amesema.

Akifungua michezo hiyo Naibu katibu mkuu Jumuiya ya Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVCC) Mussa Peter Mwakatinyo amesema Dkt Samia Cup imekuja ikiwa ni namna ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa iliyofanyika kwenye Jimbo la Same Mashariki.

Miongoni mwa mambo yaliyofanyika ni uboreshaji wa miundombinu ya Barabara, ujenzi wa madarasa kwenye sekta ya Elimu Msingi na Sekondari pia uboreshwaji wa huduma za afya na kwamba michezo hiyo inalenga pia kukuza vipaji na kujipatia ajira na kuimarisha afya kuwezesha kuendelea kuchapa kazi.

“Michezo huondoa mawazo potofu kwa vijana kama wizi na ubakaji kwa mabindi zetu hivyo kama wananchi wa Jimbo la Same Mashariki na vijana kwa Ujumla tumuunge mkono Mbuge kwani anafanya kazi kubwa kwa maslahi ya jimbo lake...

" Na kama mnavyo jionea kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuboresha huduma , jukumu kubwa la Mbunge ni kuweka msukumo kuikumbusha Serikali kwenye usimamizi wa Ilani."

Aidha ametoa pongezi kwa Mbuge Anne Kilango kwa kuanzisha mashindano haya kwa vijana wa Jimbo la Same Mashariki niimani yangu yatakuwa na tija kubwa kwakuwa wanapokutana watu tofauti hupata fursa mbalimbali kwa kubadilishana mawazo namna ya kunufaika kupitia shughuli mbalimbali.

"Hivyo kuharakisha maendeleo katika jimbo la Same mashariki na Taifa kwa ujumla, " amesema Naibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mussa Mwakatinyo.

Kwa upande wake katibu wa Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki amesema dhumuni la kuanzishwa kwa mashindano hayo ni kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa shughuli mbalimbali zilizofanyika kwenye jimbo hilo ikiwemo utekelezaji wa miradi hasa ujenzi wa vituo vya afya, ukarabati wa Barabarapamoja na uboreshwaji wa miundombinu kwenye Shule za Msingi na Sekondari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad