Na Oscar Assenga,TANGA
WATANZANIA wameshauriwa kuwa na utaratibu wa kucheki afya zao mara kwa mara kutokana na kwamba afya ndio kitu muhimu katika maisha ya kila siku.
Ushauri huo ulitolewa na Mchungaji wa Kanisa la Waadvestista Wasabato Mtaa wa Makorora Jijini Tanga Mchungaji Elinihaki Mbaga wakati akihitimisha majuma mawili ya semina ya Neno la Mungu iliyokwenda sambamba na utoaji wa huduma za kijamii.
Mchungaji Mbaga alisema kwa sababu Serikali inahitaji watu waliona na afya nzuri na Kanisa pia nalo linahitaji watu wenye afya nzuri huku akisisitiza umuhimu wa kufanya hivyo kwa ustawi wa jamii
“Katika hilo nitoe wito kwa jamii ya watanzania kuwa na uratibu wa kucheki afya zao mara kwa mara kwani hii itawasaidia kujua wanaumwa na nani na namna ya kupata tiba mapema kabla tatizo halijawa kubwa “Alisema
Huduma za Kijamii za Kitabibu zilizotolewa ni upimaji vipimo kwa magonjwa yasiyokwa ya kuambukiza ikiwemo sukari na Presha, Madaktari 5 ambao wamekuwa wakifanya huduma za kitabibu ikiwemo kutoa kipimo kwa magonjwa yasiyoambukiza.
“Tunamshukuru Mungu katika Huduma hii watu wengi wamejitokeza zoezi la upimaji wa macho watu 87 wamehudumiwa na 78 wamepewa miwani, na mwitikio umekuwa mzuri watu watu 167 wamepewa huduma mbalimbali”Alisema
Awali akizungumza Mwinjiliti Elifuraha Jonas alisema kwamba mkutano huo umekuwa wa kipekee na nzuri kutokana na huduma za kupima macho na wanatamani wakati mwengine wananchi waenda kucheki afya zao huku akieleza suala la macho limekuwa ni changamoto kwa jamii na huduma ni bure ambapo kanisa limechangia matibabu hayo ili watu watibiwe.
Hata hivyo Mwinjiliti huyo alisema wamekuwa wakibarikiwa na huduma za kiafya kutoka kwa madaktari maana wagonjwa wengi walitibiwa na walikuwa na huduma ya familia na mashauri kwenye ndoa na vijana wakihamiza wachape kazi maana Taifa linahitaji watu wachapa kazi na hata kanisa linahitaji wachape kazi.
No comments:
Post a Comment