HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 29, 2023

DC HALIMA BULEMBO APOKEA VIFAA KWA AJILI YA WATOTO NJITI

Mkuu wa wilaya kigamboni Mhe Halima Bulembo apongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa vifaa tiba walivyomkabidhi leo katika hospitali ya wilaya kigamboni ambavyo vinaenda kuanzisha wodi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

"Tumefuta kauli ya hakuna vifaa, kwasasa hatutakua na rufaa tumeletewa msaada huu wenye thamani kubwa turudishe dhumuni la wasamaria wema waliochangia kupitia Taasisi ya Doris Mollel. kwasasa tukizungumzia watoto njiti tunajivunia kazi nzuri mnayoifanya " Ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba venye thamani ya milioni 30. 

Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Lucas Davis Ngawitu amesema zaidi watoto njiti 54 wamezaliwa kutoka mwezi Januari mpaka sasa na hao wote walipewa rufaa kwenda Temeke kwa ajili ya kupatiwa huduma, tuna amini kupitia vifaa hivi tuta anzisha huduma hii hapa hapa.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad