HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 3, 2023

CHUO CHA CATC CHAFANYA MAHAFALI YA NNE YA KOZI YA UONGOZAJI NDEGE KWA KUTUMIA RADA

  



Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje amefunga kozi ya mafunzo ya Uongozaji ndege daraja la tatu kwa kuwasisitiza wahitimu kujituma katika utendaji wa kazi zao ili kuleta tija katika usafiri wa Anga hapa nchini.

Jumla ya Wanafunzi sita wamehitimu kozi hiyo ambayo itawawezesha kuongoza ndege kwa kutumia rada, kozi hii inajukana kama “Approach Control Surveillance” ni kozi ya nne tangu chuo hicho kimeanza kutumia kozi za uongozaji wa daraja la kutumia Rada.

Mafunzo hayo ya wiki saba yalihusisha masomo ya darasani kwa takribani wiki mbili na mafunzo kwa vitendo kwa wiki tano.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza na wamehitimu kozi ya mafunzo ya Uongozaji ndege daraja la tatu wakati wa mahafali ya nne ya kozi ya uongozaji ndege kwa kutumia rada yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza wakati wa mahafali ya Nne ya wahitimu wa kozi ya mafunzo ya Uongozaji ndege daraja la tatu kwa kutumia rada yaliyofanyika chuoni hapo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje
Baadhi ya Wahitimu wakikabidhiwa vyeti na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje (wa pili kulia) wakati wa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi pamoja na wahitmu wa kozi ya mafunzo ya Uongozaji ndege daraja la tatu kwa kutumia rada yaliyofanyika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad