HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 26, 2023

CHALAMILA AWAASA BANDARINI SACCOS KUWA NA WATAALAMU WA FEDHA

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS. Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila akitoa tuzo kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa bandari ya Dar Es Salaam, Mrisho Mrisho wakati wa Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023.

 Na Mwandishi wetu Michuzi TV
MKUU WA mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila amewaasa Wanachama wa Chama Cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (BANDARINI SACCOS) kuwa na watalamu wa BANDARINI SACCOS iweze kwenda vizuri wanahitaji watu wenye taaluma ya fedha na wabunifu ambao wanaweza kupeleka mbele Saccos hiyo pia inahitaji viongozi wanaoweza kuweka watu pamoja na viongozi wanaoweza kukataa kwa nguvu zote migogoro na wanaoweza kuchukua madhaifu yaliyopita na kuyabadilisha kuwa fursa. 

Hayo ameyasema leo Wakati akizungumza wajumbe wa Bandarini Saccos na jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023 katika Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS. Amesema kuwa kupitia huduma na programu mbalimbali ambazo zipo katika Bandarini Saccos inakuwa njia ya kiwaita wale wote ambao hawajajiunga ili waweze kujiunga.

Nasisitiza kwamba kwa kuwa kunamanufaa ambayo tumeelezwa na viongozi, wale wote ambao hawajajiunga muda muafaka sasa wa kujiunga kwa sababu SACCOS hii inaviongozi bora." Amesisitiza

Pia amewasisistizia kuwa wawazi wanapofanya jambo lolote kwani ndio msingi wa kila kitu kwa maendeleo ya BANDARINI SACCOS.

"Natamani kuona mwakani wanachama wa Bandarini saccos wanaongezeka zaidi kutokana na huduma nzuri zinazotokana na Saccos hiyo. 

Pia amewaasa kuachana na biashara nyingine za ununuaji wa viwanja na kujenga majengo watapoteza mweleko.

"Waangalie namna bora ya kuuza fedha kwa wanahisa na kwa watu wote wanaohitajika, pamoja nakutanua wigo wa wajumbe wengine kujiunga ndani ya SACCOS ili kuweza kupata makuzi makubwa ambayo itakuwa na tija."  Amewasisitizia

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania, Ernest Nyambo akizungumzia mafanikio ya Saccos hiyo amesema teyari wameshajenga ofisi ya kudumu karibu na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Temeke.
Mkurugenzi wa bandari ya Dar Es Salaam, Mrisho Mrisho akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa Mamalaka ya Bandari Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania, Ernest Nyambo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023. 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania Justicia Masinde akitoa mikono kwa meza kuu mara baada ya kupokea cheti cha kutambua Mchango wake wakati wa akati wa Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania, Ernest Nyambo akipokea chati wakati wa Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023. 

 




Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari na wanachama wa Chama Cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania,wakiwa katika Mkutano Mkuu wa 55 wa Mwaka 2023 wa Chama Cha BANDARINI SACCOS mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2023. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad