HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2023

CATC yafanya mahafali kwa wanafunzi wa kozi za usafiri wa anga kutoka Tanzania na Uganda


Wanafunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) wameaswa juu ya umuhimu wa kukumbuka kwamba kusoma ni safari na ukamilifu wake ni kuonyesha umahili baada ya masomo husika.

Hayo yamesemwa na Brigedia Generali Stephen Kiggundu Kamanda Msaidizi kutoka Jeshi la Anga la Uganda akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo cha CATC jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2023 na kuongeza kuwa walimu hutoa mwangaza tu hivyo ni jukumu la wanafunzi kusoma zaidi.

Brigedia Generali Kiggundu ameipongeza CATC kwa jitihada zake za kutoa mafunzo kwa wanafunzi kutoka Uganda kitendo ambacho sio tu kinaimarisha shughuli za usafiri wa Anga za Uganda bali pia kinaimarisha anga zima la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Brigedia Generali Kiggundu pia amewapongeza wahitimu kwa kuonyesha juhudi katika masomo yao na wote kufaulu vizuri.

Jumla wanafunzi 10 wamehitimu ambapo miongoni mwao watatu ni kutoka nchini Uganda ambao wamehitimu kozi namba 45 ya masomo ya Usimamizi wa utoaji wa Taarifa za Anga ‘Aeronautical Information Management’ na wengine saba wamehitimu kozi namba moja ya Usimamizi wa Kudhibiti Wanyama hatarishi katika usafiri wa Anga ‘Aerodrome Wildlife Hazards Management’ kutoka Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) na Zanzibar(ZAA).

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha CATC Aristid Kanje aliwakumbusha wahitimu hao juu ya umuhimu wa kuleta mabadiliko chanya pindi wanaporudi kwenye maeneo yao ya kazi na kuongeza kuwa menejimenti zao zitawapatia tena fursa za kusoma zaidi pindi watakapoona kuna mabadiliko kutoka kwao.

Chuo cha CATC ni chuo kinachotoa mafunzo ya kozi za muda mfupi katika usafiri wa anga nchini kinachotambulika kitaifa na Kimataifa na kina ithibati za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTvet) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) ambapo ni mwanachama kamili wa ICAO Trainair Plus katika kiwango cha Gold.
Kamanda Msaidizi kutoka Jeshi la Anga la Uganda Brigedia Generali Stephen Kiggundu  pamoja na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu, wageni kutoka Uganda na wafanyakazi wa Chuo hicho mara baada ya kumalizika kwa mahafali hayo.
Kamanda Msaidizi kutoka Jeshi la Anga la Uganda Brigedia Generali Stephen Kiggundu akizungumza na wahitimu pamoja na wafanyakazi wa  Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) wakati wa mahafali ya  kozi namba 45 ya masomo ya Usimamizi wa utoaji wa Taarifa za Anga ‘Aeronautical Information Management’ na  kozi namba moja ya Usimamizi wa Kudhibiti Wanyama 

Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi  Kamanda Msaidizi kutoka Jeshi la Anga la Uganda Brigedia Generali Stephen Kiggundu kwa ajili ya kutoa nasaha zake kwenye mahafali ya chuo hicho.
Baadhi ya wahitimu wa kozi namba 45 ya masomo ya Usimamizi wa utoaji wa Taarifa za Anga ‘Aeronautical Information Management’ na  kozi namba moja ya Usimamizi wa Kudhibiti Wanyama wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika chuoni hapo.
Kamanda Msaidizi kutoka Jeshi la Anga la Uganda Brigedia Generali Stephen Kiggundu akiwakabidhi vyeti baadhi ya wahitimu wa kozi namba 45 ya masomo ya Usimamizi wa utoaji wa Taarifa za Anga ‘Aeronautical Information Management’ na  kozi namba moja ya Usimamizi wa Kudhibiti Wanyama wakati wa mahafali hayo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje.
Mkuu wa Chuo cha Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje(kulia) akimkabidhi zawadi Kamanda Msaidizi kutoka Jeshi la Anga la Uganda Brigedia Generali Stephen Kiggundu wakati wa mahafali ya chuo hicho 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad