Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jode Musica na Kibozone Pub, Bw. Denis Mutegeki amesema kuwa wakati umefika wa kuwapa wapenzi w dansi burudani ambayo wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu.
"Tumeandaa Tamasha hilo ili kuweza kuwapa wapenzi wa dansi burudani ya uhakika ambayo wamekuwa wakiikosa kwa muda mtefu kwa vile hao wanamuziki ni mara chache sana kuwakuta pamoja kwa vile kwa sasa wamekuwa wanapiga katika bendi zao," amesema Mkurugenzi Mutegeki.
Amesema kuwa wanamuziki hao watatoa burudani kwa muda wa saa 5 bila kupumzika kwa vile wananyimbo nyingi za kutosha.
Kwa upande wake Mwanamuziki Tarsiss Masela amewakaribisha wapenzi wa muziki wa dansi kujumuika nao katika Tamasha.
Ameongeza kuwa Akudo Impact Reunion itawajumuisha wanamuziki wote waliounda kundi la Akudo Impact wakati huo akiwemo yeye mwenyewe Tarsiss Masela, Christian Bella, Fabric Kulialia, Zagreb pamoja na Katoto Maya.
Tamasha hilo limeandaliwa na Kibozone Pub.
No comments:
Post a Comment