HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 26, 2023

WIZARA YA KILIMO YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WADAU WA KILIMO

fisa Mdhamini Wizara ya Kilimo Pemba Mhandisi Idris Hassan Abdulla akizungumza na Waandishi wa habari katika ziara ya kuangalia utekelezaji wa mradi wa Agri-connect. 

Na Fauzia Mussa , Maelezo

WIZARA ya Kilimo ,Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar imesema uwepo wa miradi ya kilimo kunapelekea kuikomboa jamii kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ziara ya wadau wa mradi wa Agri connect kuangalia utekelezaji wa mradi huo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo Pemba Mhandisi Idris Hassan Abdulla amesema kupitia mradi huo jamii imeweza kunufaika kwa kujiongezea kipato pamoja na kupata lishe nzuri kwaajili ya familia.

Alifahamisha kuwa Mradi huo una lengo la kuwainua wakulima wa mbogamboga , viungo,pamoja na wajasiriamali wanaojishuhulisha na utengenezaji wa majani ya chai na kahawa,hivyo Wizara itaenedelea kuunga mkono juhudi za wadhamini wa mradi huo ili kufikia malengo yalioyotarajiwa.

Mapema ameishukuru Jumuiya ya umoja wa ulaya kwa kuwekeza fedha zao katika mradi huo unaolenga kutoa ajira hasa kwa wanawake na vijana.

Kwa upande wake Meneja Mkuu mradi wa viungo Simon Makobe alisema lengo la ziara hiyo ni kuangalia changamoto zinazowakabili watekelezaji wa miradi ya agri connect na kuweza kuzipatia ufumbuzi.

Aidha aliishukuru Wizara ya Kilimo kwa kusimamia shughuli zote zinazofanyika chini ya mradi huo pamoja na Jumuiya ya Ulaya ambayo imeamini kutoa fedha na kuziwekeza kwa wajasiariamali wakiwemo wakulima wa mbogamboga, matunda na viuongo.

Sambamba na hayo aliwataka wakulima kushirikiana kwa pamoja katika kilimo kwa kuzalisha bidhaa zinazofanana ili kurahisisha kupata masoko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Katibu wa kikundi cha Tumaini la Kijani Ali Shauri na mkulima wa Viungo Aviwa walisema kwasasa wamekuwa wakipunguza gharama za matumizi kwaajili ya mlo kwani kilimo kinawasaidia kupata mahitaji ya chakula na mbogamboga.

"Sasahivi kina mama hawanunui tena mboga,tungule ,bamia,wala nyanya zote tunapata kupitia bustani zetu za nyumbani"Katibu huyo

Walisema kupitia mradi huo jamii imepata elimu juu ya mbinu bora za kilimo hai hivyo kwasasa wanajipatia chakula salama kwani wanarutubisha vilimo vyao kwa kutumia mbolea asili ikiwemo kinyesi cha Ng’ombe.

Aidha walisema awali jamii ilikua ikipanda bustani za maua kama pambo lakini baada ya kupata elimu wameanza kupunguza upandaji wa maua na wengine kuoondoa kabisa nakuweka bustani za mbogamboga (kitchen garden ) pembezoni mwa nyumba zao ili kupunguza gharama za mlo.

Hivyo waliwashauri Vijana na Wanawake kuacha kukaa bila ya kujishughulisha na badala yake kujiunga na vikundi vya ujasiriamali na kuanzisha kilimo kitakachowapatia kipato na kupunguza gharama za maisha.

Mbali na mafanikio hayo wakulima hao wanakabiliwa na uhaba wa maji,pamoja na masoko ya nje.

Ziara hiyo iliyoambatana na ujio wa ujumbe wa jumuiya ya umoja wa Ulaya ,watekelezejai wa miradi ya Agri connect Zanzibar na Tanzania Bara, timu ya ushauri wa mradi Tanzania wakishirikiana na Wizara ya kilimo na fedha Zanzibar ilifanikiwa kutembelea kikundi cha Tumaini la kijani Chuini,Shamba la Viungo na matunda Kizimbani na kiwanda cha kutengeneza majani ya Chai Amani Zanzibar.
Katibu wa kikundi cha Tumaini la kijani Ali Shauri akizungumza na wafadhili wa mradi wa agriconnect kuhusiana na bustani za nyumban (kitchen garden) wakati walipowatembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo,huko Chuini Wilaya ya Magharibi “A”.
Mkulima wa viungo(spices) na matunda Aviwa akielezea maendeleo ya kilimo hicho wakati alipotembelewa na wadau wa mradi wa Agri connect huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad