HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 14, 2023

Waziri Jenista Mhagama akoshwa na Mshiko Fasta ya NMB

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amewataka vijana kuchangamkia fursa ya mkopo wa Mshiko Fasta unaotolewa na benki ya NMB katika kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo Mkoani Manyara kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa yanayoendelea Wilayani Babati, alipotembelea banda la Benki ya NMB.

Waziri Mhagama alisema kuwa mkopo wa Mshiko Fasta umejipambanua katika malengo makubwa ya maadhimisho hayo ambayo ni kutatua changamoto wanazokumbana nazo vijana ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

Akimuelezea Waziri Mhagama kuhusu Mshiko Fasta, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus alisema kuwa wamefikia kubuni huduma hiyo ya Mshiko Fasta kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wao wanaofanya shughuli za kiujasiriamali kupata fedha za haraka kupitia simu zao za mkononi.

“Huduma hii inalenga kuwasaidia wajasiriamali kupata mkopo wa haraka kupitia simu zao za mkononi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kila siku. Mteja wa Benki ya NMB ataweza kukopa mpaka shilingi 500,000 bila kufika tawini na wala kuweka dhamana yeyote." Alisema Baraka

Aidha Baraka alielezea zaidi kuwa NMB ina masuluhisho mbalimbali mbayo yanalenga vijana na kuwapa nafasi vijana kutumia huduma hizo kwaajili ya kunufaika zaidi ikiwemo huduma ya Spend to save ambayo inahamasisha uwekaji wa akiba, lakini pia wanaendelea kuwakaribisha vijana waweze kuwekeza kupitia hati fungani ya NMB Jamii yenye riba nzuri ya asilimia 9.5 kwa mwaka kwa manufaa yao ya baadae.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amesema kuwa, lengo la maadhimisho hayo ambayo yamedhaminiwa na Benki ya NMB ni kuwawezesha vijana kupata jukwaa la kujadili fursa zinazozotolewa na Serikali na kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira. Aliishukuru pia NMB kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanawawezesha vijana kujikwamua zaidi kiuchumi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama akimweleza jambo Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini - Baraka Ladislaus alipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa Wilayani Babati, Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini - Baraka Ladislaus alipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa Wilayani Babati, Manyara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad