HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 30, 2023

Wateja watano washinda fedha taslimu kupitia droo ya Kopa Tukubusti ya Benki ya Letshego Faidika

  Jumla ya wateja watano wa benki ya Letshego Faidika wameshinda zawadi  za fedha taslimu kupitia droo ya kampeni ya mpya ya Kopa Tukubusti.

Wateja hao ni Lucas  Skale wa Kaliua aliyeshinda sh 1,042,500, Spear Malipotea  wa Babati aliyeshinda sh3,015, 000 na Pamela Kenyuko wa Ushetu  aliyeshinda sh187,533.

Wengine ni Issa Kitangu wa Kasulu aliyeshinda sh 147,872na Fatuma Lugongo aliyeshinda sh 133,141.

Wateja hao wameshinda kiasi tofauti cha fedha baada ya kukopa fedha ambapo benki hiyo uwazawdia  asilimia 50 ya kiasi cha fedha waliyokopa baada ya kuchezesha droo kila baada ya wiki mbili.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa aliwapongeza washindi hao kwa kujipatia fedha hizo ambazo uwekwa kwenye akaunti ya mshindi moja kwa moja.

Nalingigwa alisema kuwa kampeni hiyo inazidi kushika kasi na kuwaomba wateja wao kuchangamkia mikopo yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kuweza kusaidia kugharimia mahitaji mbalimbali.

Benki hoyo imetenga kiasi cha Sh50 billion kwa ajili ya kuwazawadia wateja wao kupitia kampeni hiyo.

 “Tumeweka jumla ya Sh50 biliioni kwa ajili ya kukopesha wateja wetu. Mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya Kopa Tukubusti. Lengo hapa ni kubadili maisha ya wateja wetu. Kwa mfano, mteja  anaweza kukopa mpaka kiasi cha Sh milioni 150 ambapo akishinda kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti, atazawadiwa Sh milioni 75,” alisema Bw. Nalingigwa.

Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.

Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru aliipongeza benki ya Letshego Faidika kwa kuendesha droo hiyo ambayo inawafaidisha wateja wake.

Mfuru alisema kuwa droo hiyo imekidhi vigezo vyote na kuwaomba wateja wa benko hiyo kuchangamkia fursa hiyo ili kunufaika nayo.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) akizungumza wakati wa droo ya kutafuta washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru.


Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) akisisitiza jambo wakati wa droo ya kampeni ya Kopa Tukubusti. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru. Madhumuni ya kampeni Kopa Tukubusti ni  kuwafaidisha wateja wa benki hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha  Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa (kulia) akimsikiliza kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru. Madhumuni ya kampeni Kopa Tukubusti ni  kuwafaidisha wateja wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad