HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 24, 2023

URUSI YASIFIA USHIRIKIANO WAO NA TANZANIA

 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BALOZI wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan amesema ushirikiano uliopo baina ya nchi yao na Tanzania ni mzuri ambapo unasaidia pia kuleta na kukuza maendeleo ya uchumi baina ya mataifa hayo mawili kupitia sekta mbalimbali.

Akizungumza kwenye Kongamano mahsusi lililoandaliwa kuonyesha ‘Robots’ kwa Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya Sayansi, Mhe. Avetisyan ushirikiano huo utasaidia pia kuleta maendeleo endelevu kupitia matumizi ya teknolojia hizo za kisasa.

“Tunamshukuru sana Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ameonyesha ushirikiano na uhusiano mzuri baina yetu sisi kama mataifa, sisi Urusi tutaendelea kushirikiana na Tanzania katika kila sekta za maendeleo,” amesema Mhe. Avetisyan

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Lugha ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Mutembei amewataka vijana wa Tanzania wanaosoma masomo ya Sayansi kutumia fursa hizo za ushirikiano na taifa la Urusi ambayo wanaleta teknolojia hiyo ya ‘robots’

“Kupitia teknolojia hizo zinazoletwa na wenzetu waliopiga hatua kwenye maendeleo, tunawasihi vijana wetu watumie teknolojia hizi kama hawa ‘robots’ kwenye Kilimo kwenye masuala ya Afya,” amesema Prof. Mutembei.

Naye, Shujaa wa Urusi, Mwanaanga mstaafu wa Urusi na Mkongwe aliyekwenda anga za juu mara nne, Anton Shkaplerov amesema teknolojia hizo za ‘robots’ zitasaidia vijana wa Tanzania kuisaidia nchi yao kupiga hatua za maendeleo katika Sekta mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad