HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 5, 2023

TCD, VIJANA, WATU WAZIMA, WAZEE WA VYAMA NCHINI WABADILISHANA UZOEFU NA MAARIFA KISIASA

Mwenyekiti wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza wakati wa kufungua mazadiliano rika kwa vijana na watu wazima na wazee katika mkutano uliofanyika leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KITUO Cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimekaa kwaajili ya kufanya majadiliano rika baina ya viongozi wa vyama vya siasa wa rika mbalimbali wakiwemo Vijana wenye umri wa kati pamoja na wazee kwaajili ya kubadilishana uzoefu na maarifa ya uongozi baina yao.

Lengo la majadiliano hayo ni kuwaongezea maaarifa vijana ili waweze kuwa na ushiriki wenye tija katika mchakato wa kisiasa na Uongozi hapa nchini.

Akizungumza na wakati wa kufungua Majadiliano hayo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5, 2023, Mwenyekiti wa TCD, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa vijana wanatakiwa kuwa na uwezo ili waweze kushiriki katika shughuli za kisisa
Kwasababu mambo muhimu katika maendeleo ya nchi na malengo makuu ya maendeleo yanawahusu vijana.

"Sauti ya vijana kwenye maamuzi ni mhimu sana na kuweza kupata sera muafaka na utekelezaji muafaka katika mambo ambayo yanawagusa vijana."

"Ili vijana sauti zao ziweze kusikika ni mhimu kuweze kuwa na mfumo wa demokrasia ya kweli, kwamba watu wanapoenda kupiga kura, wanawachagua vijana ambao watasimamia utekelezaji wa sera zinazotatua matatizo ya vijana, basi zile kura za vijana na kura za wapiga kura wote ziwaendee wale watu ambao vijana wamewachagua." Ameeleza Prof. Lipumba

Amesema kuwa jambo la Msingi la kuweza kujenga msingi wa demokrasia ni kujenga uwezo wa vijana kushiriki katika shughuli za kidemokrasia na katika chaguzi za kisiasa, kupiga kura lakini pia kama wagombea wa nafasi mbalimbali.

Amesema Uzoefu wa wazee na watu wazima, ushiriki wao katika siasa wakati wakiwa vijana na ushiriki wa vijana ni tofauti, vijana wana matatizo yao, lazima vijana waeleezwe bayana ili kufahamishana namna ya kuweza kuwa wavumilivu katika shughuli za kisiasa, namna ya kujengeana uwezo ili ushiriki uwe mkubwa na wao wawaeleze wazee mambo ya kimfumo ambayo yanahitaji kurekebishwa ili ushiriki wao uweze kuwa chanja na ushiriki kamilifu katika ujenzi wa wa demokrasia nchini.

Akizungumzia kuhusiana hali ya demokrasia nchini kama inatoa uwanja wa vijana kushiriki katika siasa, Prof. Lipumba amesema kuwa kwa sasa demokrasia hapa nchini haitoi uwanja mpana wa vijana kushiriki katika siasa kwa sababu kama chaguzi haziaminiki kuwa za huru na haki ushiriki wa vijana unakuwa mdogo.

Lakini pia katika shughuli za kisiasa kama gharama za kufanya shughuli za kisiasa ni kubwa na vijana hawana rasilimali fedha na mali ushiriki wao unakuwa mdogo.

"Kwahiyo kunamasuala ya kimfumo yanahitaji kufanyiwa kazi kwani vijana asilimia 35 ya watanzania wote, wao wakishirikiana wakihamasishana wanakuwa na nguvu kubwa katika shughuli za kisiasa nchini na wanawaweza wakafanya maamuzi ya msingi na kuweza kuchagua watu wanaofaa na kuhakikisha kwamba mambo yanayowavusha vijana yanakuwa mbele katika sera za siasa.

Akizungumzia mifumo ya kuibadilisha ili vijana washiriki katika shughuli za uchaguzi, Prof. Lipumba amesema kuwa mifumo ya kubadilisha ni tume huru ya uchaguzi, kuwa na katiba ambayo itatoa utaratibu wa vijana kushiriki katika shughuli za kisiasa na za uongozi katika nchi na kutoa mawazo yao.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa NCCR MAGEUZI taifa, Elisante Ngoma amesema kuwa hali ya demokrasia nchini imeanza kuimarika kwani vijana wameanza kuingia kwenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema Vyama vya siasa vinatoa nafasi kwa vijana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi...... "Tunaamini kwamba kadiri tunavyozidi kuendelea kupata elimu na tunavyoweza kubadilishana mawazo na vijana wengine wa vyama vya siasa tunapeana hamasa ya kuweza kuingia siasa na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi." Amesema
Kwa upande wa Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sumbi Omary amesema vijana wameendelea kukomaza demokrasia ndani ya ya CCM kwa miaka yote.

Amesema kukaa na vijana wa vyama tofauti ya siasa nchini wameendelea kuwapa changamoto ambazo wanazigeuza kuwa fursa kwasababu hawazibezi na wanazipokea na wameendelea kuwasisitiza vijana wenzao kujibizana kwa hoja.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Vijana TCD na Katibu mkuu wa wa Vijana CUF, Idd Mkanza amesema kuwa amesema kuwa hali ya ushiriki kwa vijana kwenye siasa ni nzuri lakini kuna mambo ya msingi yakifanyika yataongeza ushiriki wa vijana kwenye siasa.

i. Kupitia miswada mbalimbali hasa mswada wa sheria za vyama vya siasa inayopelekwa bungeni.

ii. Uwiano sahihi wa viongozi katika siasa, kama mwenyekiti akiwa kwenye kundi la wazee na makamu mwenyekiti awe kundi la vijana na mawazo ya vijana yataweza kufika katika ngazi ya juu au sehemu ambazo zinahitajika.

iii. Vijana wenye kuanzia miaka 18 wasishiriki tuu kupiga kura lakini washiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi

iv. Kuwa na baraza la vijana ambalo litaunganisha vijana wenye vyama na wasio kuwa na vyama kwaajili ya kusukuma ajenda za vijana.

Amesema vitu hivyo vikifanyika vitaongeza ushiriki mpana wa vijana kushiriki katika ngazi mbalimbali hasa za kutunga sheria kwenye ngazi za maamuzi.
Naibu Katibu Ngome ya VijanaTanzania Bara, ACT WAZALENDO, Sevelina Mola amesema kuwa vijana wanatakiwa kujua cha kufanya ili kufikia na kuleta maendeleo nchini.
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Pambalu amesema amepongeza jitihada zilizoanzishwa na TCD, kwa kuwakutanisha na vizazi rika katika mkutano huo unaweza kuimarisha demokrasia ya nchi kwasababu wamewaunganisha vijana kupitia viongozi vijana wa vyama vya siasa.

Amesema kubadilishana uzoefu huko na maarifa kutawasaidia vijana kujenga ujasiri wanamna ya kushiriki katika vyama vyao shughuli za kisiasa kati ya vijana na vizazi rika waliowazidi na vijana wenye umri mdogo zaidi.

Amesema kuwa kiwango cha ujasiri kitaongezeka kwa namna ya kufanya siasa ndani ya vyama na kuangalia namna wakubwa wao wanavyofanya siasa na ni namna gani wameweza kukua kisiasa na kukaa kwa muda mrefu na kufanikisha sehemu ya malengo yao.
Mwenyekiti wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mazadiliano rika kwa vijana na watu wazima na wazee katika mkutano uliofanyika leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCD, Benadetha Kafuko, akizungumza wakati wa kufungua mazadiliano rika kwa vijana na watu wazima na wazee katika mkutano uliofanyika leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam.Vijana wakimsikiliza Mwenyekiti wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa kufungua mazadiliano rika kwa vijana na watu wazima na wazee katika mkutano uliofanyika leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam.

Picha za pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad