HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 11, 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

Tanzania Commercial Bank jana iliungana na mataifa mbalimbali duniani kote kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa mteja kwa mwaka 2023 ilikuwa na kaulimbiu ya “TEAM SERVICE” hiyo huku benki hiyo ikijikita zaidi na dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora na zinazokidhi mahitaji ya wateja.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki wa huduma kwa wateja Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo ambaye ni mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya alisema benki ya TCB inachukulia kwa ukubwa wa hali ya juu sana kutoa huduma kwa wateja ndiyo maana kwa Tanzania commercial bank huduma ni moja ya mikakati na utamaduni wa benki hiyo.


Msuya alisema “kaulimbiu ya mwaka huu inaendana hasa na utekelezaji wa majukumu yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu wa Tanzania Commercial Bank na kuboresha huduma ni hamasa ya biashara na TCB imeweka kipaumbele cha kutoa huduma bora kwa wateja”.

"Hii ndiyo sababu Tanzania Commercial Bank inaendelea kuwekeza mara kwa mara katika jamii na kuwapa wafanyakazi wetu ujuzi na rasilimali zinazohitajika ilikuhakikisha wanawapa wateja wetu huduma za hali ya juu," Msuya alisema. 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja. Hafla hiyo ilifanyika katika tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni ambapo ilikuwa na kaulimbiu ya "TEAM SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki yake kuendelea kutoahuduma bora kwa wateja wake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati) akikata keki pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja katika tawi la Mlimani City jijini Da es Salaam. hivi karibuni ambapo ilikuwa na kaulimbiu ya "TEAM SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki yake kuendelea kutoahuduma bora kwa wateja wake.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki hiyo

Baadhi ya maofisa wa Tanzania Commercial Bank pamoja na wateja wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad