HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 31, 2023

TAKUKURU RAFIKI YAOKOA MIL.4 ZA SERIKALI YA KIJIJI CHA KANGA MAFIA

 

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
KAIMU Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani, Bakari Alli amesema kuwa wamefanikiwa kuokoa kiasi cha Mil.4 kwa kupitia mikutano ya TAKUKURURAFIKI Wilayani Mafia Mkoani Pwani.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Oktoba 31 kwenye Ukumbi wa mikutano ofisini hapa ,amesema.

" Programu ya TAKUKURU Rafiki ayo hufanyika wazi katika mikutano ya kata jambo linalowajengea uwezo wananchi kuibua kero ambazo endapo zikiachwa ziendelee zinaweza kusababisha vitendo vya kushamiri zaidi rushwa nchini" amesema Bakari.

"TAKUKURU Rafiki imezaa matunda Wilayani Mafia ambapo wananchi wameibua kero kuwa Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Kanga ambaye kwa nafasi yake ni Afisa Mazingira wa Kata hiyo kuwa alifanyia ubadhirifu wa Sh.Mil. 4 fedha zilizotokana na mauzo ya kiwanja cha ufukweni ambapo fedha hiyo ilikuwa ni tozo asilimia tano (5%) ya mauzo ya kiwanja na fedha hiyo ilikuwa ni mali ya serikali ya Kijiji cha Kanga kilichopo Kata ya Kanga" amesema.

"Baada ya Afisa Mazingira huyo kupokea fedha hizo hakukiwasilisha Ofisini wala hakuiweka katika akaunti ya Benki ya Kijiji badala yake aliitumia kwa manufaa yake binafsi, ndipo kwenye mkutano wa TAKUKURU Rafiki wananchi waliibua kero hiyo na makubaliano yaliwekwa kuwa TAKUKURU ifuatilie suala hili na endapo ikibainika ni kweli Afisa mazingira arejeshe fedha hizo" amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki.

Amesema kuwa baada ya uchunguzi imebainika kuwa ni kweli na tayari ameirejesha fedha hiyo kwenye akaunti ya Kijiji cha Kanga hivyo tayari TAKUKURU imemwandikia barua mwajiri wake kumtaarifu suala hili ili achukulie hatua.

Kazi nyingine zilizofanyika katika ni kama ifuatavyo uzuiaji rushwa utekelezaji miradi ya maendeleo.

" Tumefanya kazi ya ufuatiliaji miradi 48 ya maendeleo yenye thamani ya Bil. mia tano tisini na nane laki mbili na tisini na mbili elfu na shilingi themanini na nne na senti tisi na nne (9,598,292,084.94) katika sekta za Elimu, Afya, Maji, na Barabara", amesema Sadiki.

Aidha katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo, baadhi ya miradi imebainika kuwa na mapungufu na hatua zimechukuliwa.

Amesema kuwa tayari wameweka mikakati ya kudhibiti mianya ya rushwa na vikao hivyo vitafanyika katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu.

Amesema mikutano ya hadhara 48 imefanyika semina 48, kwa watumishi wa serikali na sekta binafsi ziefanyika onesho moja limefanyika, klabu za wapinga rushwa 67 zimeimarishwa kwenye Shule za Msingi na Sekondari.

Aidha elimu dhidi ya rushwa imetolewa kupitia vipindi vitatu vya redio amesema Kaimu Kamanda Sadiki.
" Idadi ya malalamiko yaliyopokelewa yanayohusu rushwa huku yasiyohusu rushwa yamehamishiwa idara nyingine kati ya malalamiko 126, malalamiko 92 yalihusu rushwa majalada yamefunguliwa na uchunguzi umeanza pindi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.

" Malalamiko 34 hayakuhusu rushwa, Katika malalamiko 34 yasiyohusu rushwa 04 yamefungwa matatu yamehamishiwa Idara nyingine na 19 walalamikaji wameshauriwa na 8 uchunguzi wa awali unaendelea.

Amechanganua malalamiko hayo kisekta kuwa ni afya,ardhi, bandari, biashara binafsi,ofisi ya Mkuu wa Wilaya , elimu,kilimo,madini.

Hadi sasa mashauri mapya yaliyoamuliwa yaliyoshinda yaliyoshindwa 7, 6 3 3.

TAKUKURU Mkoa wa Pwani Wamepanga kuendelea na kampeni ya kutokomeza rushwa na matumizi ya madaya ya kulevya iliyozinduliwa kwa ushirikiano kati Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya, kwa lengo la kuelimisha jamiii kutokomeza rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya itakayotekelezwa kuanzia Shule za Msingi, Sekondari hadi Vyuo sambamba na

kuendelea kufanya ufuatiliaji na chambuzi za mifumo kwa lengo la kuziba mianya ya rushwa itakayobainika.

Kuendelea kukagua utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo katika mkoa wetu kuendelea na uchunguzi wa vitendo vya rushwa na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale watakaobainika kutenda makosa ya rushwa.

Kaimu Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi na wadau wote katika Taasisi za serikari na sekta binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za mapambano dhidi ya rushwa kwa kukataa kujihusisha na vitendo vya rushwa na madawa ya kulevya, kuendelea kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili thamani ya fedha ya serikali ionekane na kwa kufanya hivyo miradi ya maendeleo itatekelezwa kwa kiwango kilichokusudiwa na hivyo kuleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.

"Waananchi ni wajibu wao kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa endepo utavishuhudia au kusikia ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria" amesema Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki .

"Natoa onyo kwa wale watakao haribu miradi ya maendeleo kwa uzembe au makusudi hatutawafumbia macho tutaendelea kuchukua hatua kali za kisheria" amesema.

Amesema katika kupambana na rushwa wanayo kaulimbiu isemayo “kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu" amesema Sadiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad