Shirika la Elimu Kibaha (KEC) limepokea wanafunzi wapya 46 kutoka katika Chuo cha Biashara Kibaha (KIB) kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya kozi za muda mfupi wa miezi miwili.
Katika kipindi cha miezi miwili Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha- FDC) kitatoa mafunzo ya urembo na ususi, hotelia, ufundi magari, mapambo, ushonaji na ubunifu wa mitindo kwa wanafunzi wa Chuo cha Kibaha Institute of Business.
Akifungua mafunzo hayo, mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anathe Nnko amekishukuru Chuo cha biashara Kibaha (KIB) kwa kuchagua Shirika la Elimu Kibaha kupitia Kibaha-FDC, kwa kuwapeleka wanafunzi wa KIB kupata mafunzo Kibaha-FDC.
Bw. Nnko aliwashauri wanafunzi wa KIB kufanya mafunzo kwa vitendo ili kujiimarisha wakati wakipatiwa mafunzo hayo lakini pia waweze kujiajiri na kuajiri watu wengine baada ya kumaliza mafunzo hayo.
“Nidhamu ni sehemu ya mafanikio, nidhamu itawasaidia kokote mtakapokuwa, sisi tumejipanga kutoa mafunzo bora,” amesema Bw. Nnko.
Mmiliki wa Chuo cha Biashara Kibaha (KIB), Prof. Lemayon Melyok amekishukuru Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha kwa kukubali kuwapokea wanafunzi wa chuo chake.
“Sisi tuliona kuwa wanafunzi wetu wakija kusoma hapa Kibaha watakuwa salama kwani watapata elimu ya nadharia na vitendo,” amesema Prof. Melyok.
Mratibu wa Mradi wa AHADI wa World Vision, Bi. Eveline Sanga amewataka wanafunzi hao kuwa makini darasani kwani mafunzo hayo yatawasaidia kupata kipato ambacho kitawasaidia kuboresha maisha yao.
Mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha, Asha Njoroka aliwakaribisha wanafunzi wa KIB na kuwataka kuwa na ushirikiano wakati wa mafunzo hayo.
Naye, mwanafunzi wa KIB, Rosemary Emily aliahidi kutoa ushirikiano kwa walimu na wanafunzi wa Kibaha- FDC.
Shirika la Elimu Kibaha kupitia Kibaha-FDC limewapokea wanafunzi 46, wakiwemo wanawake 30 na wanaume 16 ambao wanafadhiliwa na mradi wa AHADI wa World Vision wenye lengo la kuwakomboa kifikra na kiuchumi watoto wa umri wa miaka 13 mpaka 19.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anathe Nnko akifungua rasmi mafunzo ya kozi za muda mfupi kwa wanafunzi wa Chuo cha Biashara Kibaha. Mafunzo hayo yanatolewa katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha– FDC). Kutoka kulia ni mmiliki wa Chuo cha Biashara Kibaha, Prof. Lemayon Melyok akifuatiwa na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC), Bw. Joseph Nchimbi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Kibaha Bi. Nembris Lucas Kimbele akifuatiwa na Mratibu wa Mpango wa AHADI kutoka World Vision, Bi. Eveline Sanga.
Wanafunzi wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC), Bw. Joseph Nchimbi (pichani hayupo) katika ufunguzi wa mafunzo ya muda mfupi yanayofanyika Kibaha-FDC.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC), Bw. Joseph Nchimbi akitoa maelekezo kwa wanafunzi wapya wa Chuo cha Biashara Kibaha (KIB). Kulia ni mmiliki wa Chuo cha Biashara Kibaha, Prof. Lemayon Melyok. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Kibaha, Bi. Nembris Lucas Kimbele, Mratibu wa Mpango wa AHADI kutoka World Vision, Bi. Eveline Sanga akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anathe Nnko.
Mmiliki wa Chuo Cha Biashara Kibaha, Prof. Lemayon Melyok akitoa shukurani kwa uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) kwa mapokezi mazuri kwao na wanafunzi kwa ujumla. Kulia ni Mratibu wa Mafunzo katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC), Bw. Fidelis Maziku. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anathe Nnko akifuatiwa na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC), Bw. Joseph Nchimbi.
Mratibu wa Mpango wa AHADI kutoka World Vision, Bi. Eveline Sanga akiwasisitiza wanafunzi kuwa nafasi waliopata ni Neema hivyo waitumie vizuri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anathe Nnko na kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Biashara Kibaha, Bi. Nembris Lucas Kimbele.
Wanafunzi wapya kutoka Chuo cha Biashara Kibaha (KIB) wakitambulishwa kwa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha- FDC).
Walimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha na Walimu wa Chuo cha Biashara Kibaha wakitambulishwa kwa wanafunzi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anathe Nnko (alievaa kaunda suti ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Biashara Kibaha.
Wednesday, October 4, 2023
Home
Unlabelled
SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LAANZA KUTOA MAFUNZO KWA VYUO VINGINE MKOANI PWANI
SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LAANZA KUTOA MAFUNZO KWA VYUO VINGINE MKOANI PWANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment