HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 13, 2023

SERIKALI IMELIKUMBUSHA SHIRIKA LA WAKIMBIZI UMUHIMU WA KURASIMISHA SHUGHULI ZA KIBINADAMU

 NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, amelikumbusha Shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi (UNHCR) kuhusu umuhimu wa urasimishaji wa shughuli za usaidizi wa kibinadamu (Localization of Humanitarian Assistance) kwa kuzipa nafasi na kipaumbele NGO’s za ndani ya nchi ili kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za hifadhi ya ukimbizi.


Ameyasema hayo leo Oktoba 12, 2023 wakati wa Mkutano wa 74 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) unaofanyika Geneva – Uswisi, akichangia hoja wakati wa mjadala wa kupitisha taarifa za kiutawala, program, bajeti na usimamizi wa fedha za Shirika la UNHCR.

Mhe. Sagini Aliongeza kuwa NGO’s za ndani ndio za kwanza kutoa usaidizi wa kibinadamu wakati wa majanga na pia zinaelewa mazingira ya kiujumla ya nchi na hivyo kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kikamilifu, kwa kuzingatia mahitaji ya eneo husika na hivyo kuepusha mivutano baina ya wakimbizi na Wananchi wenyeji.

Aidha Mhe. Sagini, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu Msaidizi wa Ofisi inayoshughulikia Idadi ya Watu, Wakimbizi na Wahamiaji (Bureau of Population, Refugees, and Migration) nchini Marekani Bi. Elizabeth Campbell kuhusu hali ya hifadhi ya ukimbizi nchini Tanzania.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembeni ya Mkutano wa 74 wa Kamati Tendaji ya UNHCR unaoendelea Geneva – Uswisi.

Sambamba na hayo Mhe. Sagini aliishukuru nchi ya Marekani kwa kuendelea kufadhili shughuli za hifadhi nchini pamoja na kuipunguzia mzigo Tanzania kwa kuhamishia nchini Marekani wakimbizi zaidi ya 5000 tangu mwezi January mwaka 2023.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad