HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2023

NAMTUMBO WOMEN FORUM KUWABADILISHA WANAWAKE KIFKRA NA KIMAWAZO

 

 

 

Na Albano Midelo,Namtumbo

WANAWAKE wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakiongozwa na
Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Ngollo Malenya wamefanya Jukwaa la
Mwanamke (Namtumbo Women Forum) lenye lengo ya kumbadilisha
mwanamke kifkra na kiuchumi.

Jukwaa hilo limefanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa Mtakatifu Agnes
Chipole mjini Namtumbo ambapo mamia ya wanawake kutoka mkoani
Ruvuma wamefundishwa mada mbalimbali za kuwajengea uwezo
kiuchumi.

Akizungumza kwenye kilele cha jukwaa hilo ambalo pia lilihudhuriwa na
baadhi ya wabunge kutoka mkoani Ruvuma,Mkuu wa Wilaya ya
Namtumbo Ngollo Malenya amelitaja lengo la Jukwaa hilo kuwa ni
kumwezesha mwanamke kiuchumi,kifkra na kimawazo ili aweze
kuibadilisha jamii inayomzunguka.

“Nilizundua Jukwaa la Wanawake wa Namtumbo Oktoba 13 ili kutekeleza
agizo la Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwenye Jukwaa hilo
zilitolewa mada mbalimbali za kumwezesha mwanamke
kiuchumi’’,alisisitiza Malenya.

Hata hivyo amesema Jukwa hilo limedhamiria kubadilisha Maisha ya
mwanamke kifkra na kimawazo ili aweze kujitambua na kupiga hatua kwa
kusonga mbele ambapo amesisitiza mwanamke kutambua nguvu
aliyonayo ili kuweza kujikimu kiuchumi na kifkra hasa katika kipindi hiki cha
uongozi wa Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Malenya amemshukuru Rais Samia kwa kupeleka miradi mbalimbali katika
wilaya ya Namtumbo ambayo amesema inakwenda kuboresha sekta
mbalimbali zikiwemo za elimu, umeme, kilimo, afya,maji,miundombinu na
maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum mkoani Ruvuma Mheshimiwa
Jakline Msongozi akizungumza kwenye kilele cha Jukwaa hilo,amewaasa
wanawake kuzingatia mafunzo ambayo wameyapata bure ambapo
amesema mafunzo hayo yanayoweza kubadilisha Maisha ya wanawake
wa Mkoa wa Ruvuma.

Amesisitiza kuwa mafunzo ya kuwejenga wanawake kiuchumi yataleta tija
katika kuendeleza familia na kukuza uchumi wa wanawake, amempongeza
Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwainua wanawake wa
Tanzania.

Naye Mbunge wa Viti Maalum wanawake mkoani Ruvuma Mheshimiwa
Mariam Nyoka amesema hii ni mara ya kwanza mkoa wa Ruvuma kufanya
tukio kubwa la Jukwaa la wanawake wa Namtumbo lililoongozwa na Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya.

Amesema Jukwa hilo limewaunganisha sio wanawake wa Namtumbo
pekee,bali wanawake wa Mkoa wa Ruvuma ambapo pia amempongeza
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo kutumia tamasha la Namtumbo
Kihenge,kutangaza fursa mbalimbali zilizopo wilayani Namtumbo.

Nyoka ameshauri wilaya nyingine mkoani Ruvuma ,kuiga mfano wa Wilaya
ya Namtumbo kwa kuhakikisha wanafanya majukwaa ya wanawake ili
kuwaendeleza wanawake ambao ni shingo ya familia.

Mheshimiwa Vita Kawawa ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo
akizungumza kwenye Jukwaa hilo ,amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu
Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni nne kujenga sekondari ya
wasichana ya Mkoa wa Ruvuma iliyojengwa wilayani Namtumbo.

Amesema sekondari hiyo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya
1000 wanaonzia kidato cha kwanza hadi cha sita imeanza kuchukua
wanafunzi mwaka huu,inakwenda kuwa mkombozi wa Watoto wa kike.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Elizabeth Ngongi amesema
jukwaa hilo limewafungua macho wanawake kutokana na mafunzo
mbalimbali waliyopata yakiwemo mafunzo ya fursa za kiuchumi,elimu ya
biashara,Saikolojia,Falsafa na Theolojia.
Mkuu wa  Wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya akizungumza wakati anatoa neno fupi kwa wanawake kwenye hafla ya Jukwaa la Wanawake wa Namtumbo kwenye ukumbi wa Mtakatifu Agnes Namtumbokatikati mwenye miwani ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Mariam  Nyoka akipolewa na wanawake wakati anaingia kwenye  ukumbi wa Mtakatifu Agnes mjini Namtumbo kwenye kilele cha Jukwaa la Wanawake wa Namtumbo (Namtumbo Women Forum ambapo mamia ya wanawake kutoka katika Mkoa wa Ruvuma wlishiriki kwenye jukwaa hiloMkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya alipolakiwa na wanawake wakati anaingia kwenye  ukumbi wa Mtakatifu Agnes mjini Namtumbo kwenye kilele cha Jukwaa la Wanawake wa Namtumbo (Namtumbo Women Forum ambapo mamia ya wanawake kutoka katika Mkoa wa Ruvuma wlishiriki kwenye jukwaa hiloMbunge wa  Viti Maalum  mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Jakline Msongozi akiwa na Mbunge mwenzake Mheshimiwa Mariam Nyoka wakizungumza kwenye Jukwaa la Wanawake NamtumboWaliokumbatiana watatu ni wabunge wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni Mheshimiwa Mariam Nyoka na Mheshimiwa Jakline Msongozi  wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma na Mheshimiwa Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo wakiwa kwenye ukumbi wa Mtakatifu Angnes Namtumbo kwenye kielel cha Jukwaa la Wanawake wa Namtumbo,wengine kulia n ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Elizabeth Ngongi na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad