HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 12, 2023

Mkoa wa Manyara unaenda Kuweka historia Oktoka 14, 2023

 

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akiongea na wanahabari.

Na Cathbert Kajuna - MMG/Kajunason, Manyara.

Mkoa wa Manyara unakwenda kuweka historia ya kuwa mwenyeji wa matukio matatu ya Kitaifa ikiwemo uhitimishaji wa Mbio za Mwenge Uhuru 2023, Ibada maalum ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2023.

Akizungumza na wanahabari mapema leo katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati, Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amesema kuwa mkoa umepata neema ya ajabu kwa kupata matukio makubwa ya kitaifa.

"Niwaombe Wananchi wa Mkoa wa Manyara pamoja na wageni wote kutoka nje ya mkoa wajitokeze kwa wingi, kwanza kumpokea Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote watakaoambatana nae katika mkoa wetu, vile vile niwaombe mjitokeze kwa wingi siku ya tukio lenyewe Katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Oktoba 14, 2023," amesema Mhe. Queen.

Mkoa wa Manyara umeanzishwa Agosti 2002 ambapo Mkuu wake wa Kwanza wa Mkoa alikuwa Kanali (mst) Anatolia Tarimo na sasa 2023 unaongo na Mhe. Queen Cuthbert Sendiga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad