Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya sita ya Promosheni ya Maokoto Deilee inayoendeshwa na Sportpesa kushirikiana na Mtandao wa Tigo imefanyika jijini Dar es Salaam, washindi watatu wamepatikana, wawili wameshinda simu janja (smartphone) na mmoja ameshinda shilingi Milioni moja.
Mshindi wa shilingi Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) ni Yassin Mustafa mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam. Washindi wa Simu janja mmoja ametoka Chamazi - Dar es Salaam, Ferdinand Kisanga na mwingine ni Juma Chande kutoka mkoani Morogoro.
Mwakilishi wa Sportpesa kutoka Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Lydia Solomon amesema oktoba 10 mwaka huu itafanyika droo ya mwisho ya promosheni hiyo ambapo mshindi wa kiasi cha fedha shilingi Milioni 15/- atapatikana, hivyo amewahimiza wateja kuendelea kubeti kupitia mtandao wa Tigo.
Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Tigopesa, Fabian Felician amesema wateja hao wanaweza kuendelea kuendelea kubashiri michezo mbalimbali kupitia mtandao huo wa Tigo na kujishindia kiasi hicho cha fedha kwenye droo hiyo ya mwisho ambapo mshindi atapata shilingi Milioni 15/-.
No comments:
Post a Comment