HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 25, 2023

MAMA'S BEACH PARTY YAFANA DAR

 

Bi. Vida Nassary Mwanzilishi wa Kitchen Party Gala, Mwanzilishi wa Tanzania Women Run Marathon, Caroline Mwanri Mtaalam wa Rasilimali Watu (former HR Director Brac), Marion Elias Mwanzilishi wa Mamas Day Out Beach Party,  Ruth Urioh mbunifu wa mavazi  Mwanamitindo J'adore Fashion Designs,  na Bw. Francis Nanai Business Consultants (a former Managing Director Mwananchi Communications Ltd & TPSF) wakiwa katika picha ya pamoja.
Mtoa mada  na Afisa Rasilimali Watu  Bi. Carolyn Mwanri akifafanua  jinsi makampuni yalivyowekeza kwenye kuhakikisha yanalinda afya ya akili ya waajiriwa wao na pia kutoa dondoo  namna gani wafanyakazi wanaweza kujilinda.
Kushoto ni Mkurugenzi wa J'adore Fashion  Bi. Ruth Urioh  na  Francis Nanai wakiwa watoa mada kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Ekima Insights na Muandaaji wa Kongamano la Mama’s Day Out Beach Party Bi. Marion Elias akitoa neno la ufunguzi kukaribisha wanenaji na wahudhuriaji katika kongamano hilo.

Na Mwandishi Wetu
MAMA's Day Out Beach Party wameadhimisha siku ya Afya ya akili kwa kuwakutanisha kina mama 170 Jijini Dar es Salaam katika Kongamano lililoandaliwa na Kampuni ya Ekima Insights inayoongozwa Mkurugenzi wake ambaye ni Mwanahabari mkongwe Marion Elius.

Kongamano hilo limefanyika hivi karibuni katika ufukwe Ununio jijini Dar es Salaam.

"Mama's day Out Beach Party imefanyika kwa mara ya pili sasa, ambapo tulianza mwaka 2022 huku lengo letu kubwa ni kutoa elimu ya kuhusu Afya ya Akili katika jamii yetu kwa kupitia wanawake kwa sababu hivi sasa kumekua na changamoto katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu ya kila siku." Amesema Marion

Mkurugezi huyo amesema kuwa kongamano hilo limefanyika sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Afya ya Akili ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 10 ya kila mwaka huku kauli mbiu yake ikiwa ni #Jikubali #AnzaUpya. #PendaMaisha." Amesema Marion.

Amesema kuwa katika kongamano hilo kulikuwa na watoa mada mbalimbali amewataja baadhi yao kuwa ni Mwanasaikolojia maarufu Dkt. Chris Mauki na wataalamu wabobevu katika masuala ya Afya ya akili ambao wametoa mada mbalimbali akiwamo Bi. Caroline Mwanri aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication na Afisa

Rasilimali watu Francis Nanai ambaye amezungumza na kuwapa mbinu wanawake juu ya suala zima la kujiimarisha kiuchumi na namna ya utunzaji wa fedha kuwekeza na pia kujiandaa na maisha ya kustaafu kwani kumekuwa na wimbi kubwa la wastaafu wengi kupoteza mwelekeo kwa sasa kwani

watanzania wengi hawana elimu ya kujiandaa na kustaafu ambayo imekuwa ikipelekea watu kupata msongo wa mawazo pindi wanapostaafu.

Mwanasaikolojia Dkt. Chris Mauki ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam amesema kuwa wanawake wanauwezo mkubwa wa kuilewa saikolojia ya mwanaume na kumudu kuwasaidia afya yao ya akili na kukuza uwezo vijana wa kiume.

Aidha Mwanamtindo na mbunifu wa mitindo ya mavazi kutoka Kampuni ya J’adore Ruth Urio amesema kuwa wanawake wapunguze kuwa na fikra zinazowapotezea muda wa kufanya masuala ya maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa Diwani kata ya Kunduchi Mhe. Michael Urioh ambaye amewasisitiza kina mama hao umuhimu wa wanawake kuwa wananafasi kubwa katika malezi ya familia na hasa ikizingatiwa tuko kwenye nyakati ambazo kuna muingiliano wa kimaadili na tamaduni toka nchi za ng’ambo, hivyo ni muhimu sana kwa wanawake kuwa jasiri na thabiti katika malezi hasa ikizingatiwa kuwa kuna ongezeko kubwa sana la watoto kulelewa na mzazi mmoja ambao wengi wao ni wanawake.

Mhe Urioh amesema kuwa serikali chini ya uongozi wa Rais wetu Mama yetu Samia Suluhu Hassan imejikita katika kumuinua mwanamke katika maeneo mbali mbali na hasa kupatiwa mikopo isiyokuwa na riba na kuhamasisha wanawake kujitokeza kutumia kikamilifu fursa hizo.

Kongamano hilo limenogeshwa na michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, kuvumbua dhahabu huku wakipata zawadi kutoka kwa Shear Illusion, GSM, J’Adore, Renex, Cassandra lingerie The Deck Resturant

Aidha muandaaji ametoa shukran kwa Taasisi ambazo waneshiriki kikamilifu ambao ni Hospitali ya Kairuki Memorial ya Mikocheni Dawasa, Coca-Cola Kwanza, Vodacom, GSM, Renex, J’Adore na wengine wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad