HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 21, 2023

OLEO LA 22 LA MBIO ZA KILIMANJARO PREMIUM LAGER INTERNATIONAL MARATHON 2024 LAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

IJUMAA OKTOBA 20, 2021: Toleo la 22 la Mbio za za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2024 limezinduliwa rasmi leo kwenye Hoteli ya Serena iliyoko Dar es Salaam kabla yatukio lenyewe kufanyika hapo Februari 25, 2024.

Akizungumza kwenye tukio lililofana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii Damasi Mfugale, aliyewakilishwa na Bw. Stephen Mpeka, alipongeza mafaniko ambayo yameshafanyika hadi sasa kwa mchango wa kutangaza utalii wa michezo.

“Tunaona fahari ya Mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon kwa sababu zimethibitisha kuwa moja ya matukio makubwa ya kimataifa katika mkoa kwa vile yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 12,000 na idadi sawa ya watazamaji kutoka zaidi ya nchi 56 na wote hawa wanaweza kuwa watalii. Haya ni mafanikio makubwa,” alisema Bw Mfugale.

Ni wakati sasa Bodi ya Utalii Tanzania iimarishe uhusiano na mbio hizi kwa kutafuta njia zaidi za kutangaza utalii wa michezo kwa vile ni wazi kwamba tukio ni jukwaa kubwa na lina wafuatiliaji wengi ndani na nje ya nchi.

“Tulisaidia Mbio za Kili miaka iliyotangulia, lakini wakati ufike sasa kuja na mawazo mapya na mazuri zaidi ili kuongeza idadi ya watalii wanaotokana na mbio za masafa marefu. Tutatangaza vivutio vyetu kikamilifu kupitia tukio hili kubwa kuhakikisha tunafikia watu wengi zaidi ndani na nje ya nchi,” alisema.

Alieleza kwamba mbio za Kili zimeongeza mchango mkubwa kwenye utalii wa michezo na hii imesaidia sana serikali kutekeleza sera za utalii na michezo.

“Nawapongeza wadhamini wote wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager (mfadhili mkuu) na Tigo -Mbio za Nusu Masafa (Kilomita 21) kwa mchango wenu mkubwa. Siwezi kuwasahau wadhamini wa meza za maji-Simba Cement, Kilimanjaro Water na TPC Sugar. Wabia rasmi – KiliMedair, Garda WorldSecurity, CMC Automobiles, Sal Salinero Hotel na wasambazaji rasmi – Kibo Palace Hotel na Keys Hotel. Bila nyinyi isingekuwa rahisi,” alisema na kuwasihi Watanzania kujiandaa kwa tukio la kimataifa ili kuhakikisha zawadi nyingi zitakazotolewa zinabaki nyumbani.

Ofisa Mtendaji Mkuu pia aliwasihi washiriki na watazamaji kutumia msimu wa Kilimanjaro International Marathon kutembelea vivutio mbalimba vya utalii kati yake kikiwemo kivutio kikubwa zaidi Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Zanzibar na vivutio vingine. Hivi siyo tu kwa watalii wa kimataifa, tuna pia vifurushi kwa watalii wenyeji.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji  wa TBL Group, Bw Jose Moran, kampuni inayozalisha, sambaza na kuuza bia, pombe mbalimbali na vinywaji visivyo na kilevi Tanzania, alisema wanaona fahari kupitia Kilimanjaro Premium Lager, mdhamini wa mbio hizo kwa miaka 22, ikifanya kampuni iwe moja ya wafadhili wa muda mrefu Tanzania. Aliongeza kwamba kwa miaka yote hii wamekuwa wakitiwa moyo kusaidia utalii na utamaduni wa Kitanzania kwa jumla - ambao tukio linasaisaidia kuutangaza.

Bw Moran alisema kwamba wametenga kiasi cha fedha zipatazo Sh28 milioni kwa ajili ya tuzo, ambapo washindi wa juu katika makundi yote mawili ya wanaume na wanawake, watazawaidiwa Sh5 milioni kila mmoja.

Aliwasihi washiriki kujisajili kwa muda unaotakiwa kwani tayari usajili unaweza kufanyika mtandaoni kupitia www.kilimanjaromarathon.com na kupitia TigoPesa.

Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo Woinde Shisael, ambaye kampuni yake inafadhili mbio za nusu masafa – (Tigo Kili hal Marathon) alisema, “kama sehemu ya kujitoa kwetu kutangaza utalii wa michezo Tanzania na kulea vipaji vya wanariadha, tunafurahi kutangaza kwamba Tigo ni mdhamini wa mbio hizo kwa miaka tisa mfululizo.

Alisema ubunifu wao wa namna ya washiriki kujisajili  kupitia Tigopesa ambapo washiriki wanaweza kujisajili kwa kupiga *150*01#, kIsha kubonyeza 5 LKS, kisha kubonyeza 5 (tiketi) na kufuata maelekezo kukamilisha usajili.”

Waandaaji wa tukio waliwasihi washiriki kutumia fursa ya punguzo la ada ya kujisajili kuanzia Oktoba 16 hadi saa sita yya usiki ya Desemba 14 na baada ya hapo ada ya kiingilio itaongezeka katika makundi yote na mataifa yote kuanzia Desemba 15 hadi saa sita usiku ya Februari 5, 2024 au hadi hapo tikiti zotezi tapokuwa zimeuzwa – yoyote itakayoanza mapema kwa vile kuna nafasi haba. Washiriki watahudumiwa kwa msingi wa anayekuja kwanza ndiye anayehudumiwa.

Waandaaji pia walisema kwamba tukio litasaidia shirika la Tumaini la Maisha (TLM) ambapo watoto wenye saratani watapata matibabu bure kwa kushirikiana na hospitali ya KCMC ya Mjini Moshi. Kwa mujibu ya waandaaji hao asilimia tano ya kila ada anayolipa mshiriki itaenda kusaidia watoto hao.

Katika mbio za mwaka huu, waandaaji walikabidhi shilingi milioni 11 zilizopatikana kutoka kwa washiriki na kukabidhiwa kukabidhiwa kwa Hospitali ya KCMC Moshi kusaidia Wodi ya Waoto wenye Saratani. “KCMC ni mbia muhimu wa mbio za masafa marefu kwa sababu ya msaada wake wa tiba kila mwaka,”alisema mwandaaji.

Mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2024 zitakazofanyika Jumapili ya Februari 25, 2024 kwenye Chuo Cha Ushirika Moshi (MoCU), zinaandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa rasmi na Kampuni ya Executive Solutions Limited. Wild Frontiers Events wana jukumu la mipango ya usafiri wa ndani na masoko ya kimataifa ya tukio hilo

 

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Stephen Mpeka (katikati) akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa mbio za Kilimanjaro Premium Lager international Marathon 2024 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Jose Moran, Katibu Mkuu ra Chama Cha Riadha Tanzania, Jackson Ndaweka, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael na Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania, Charles Maguzu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Jose Moran akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager international Marathon 2024 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
 

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager international Marathon 2024 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Stephen Mpeka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager international Marathon 2024 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad