HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 25, 2023

KFC-TANZANIA WASHEHEREKEA MIAKA 10, WAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA SERIKALI

 

 KAMPUNI ya Dough Works Limited ambao wanaendesha migahawa ya KFC-Tanzania Washeherekea Mika 10 ya kutoa huduma hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.

Katika sherehe hizo za miaka 10 pia walishiriki chakula pamoja na Watoto wenye Ulemavu kutoka kituo cha kulelea watoto wenye Walemavu Bunju cha Baba Oreste Foundation na shule ya Msingi na awali ya Rightway.

Meneja Mwendeshaji wa KFC Tanzania, Shafii Idege akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sherehe za kutimiza miaka 10 jijini Dar es Salaam, amesema kuwa KFC Tanzania imeisaidia Serikali kupunguza changamoto ya ajira pia wanatarajia kufungua migahawa mingine miaka 10 ijayo.

"KFC imetoa huduma Miaka 10 na inaendelea kuwepo kwa miaka 10 zaidi na na mambo mazuri yanakuja". Amesema

Kwa Upande wa Mlezi wa Kituo cha Kulelea Watoto wenye Ulemavucha Bunju, amesema kuwa watoto weye ulemavu wamekuwa wakisahaurika ila KFC wamewakumbuka kupata nao chakula cha mchana hii itabioresha mahusiano mema kati ya Taasisi ya elimu na watoto wenye ulemavu.Matukio Mbalimbali wakati wa     KFC-Tanzania wakisheherekea Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad