HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 12, 2023

KATIBU MKUU MSIGWA ATEMBELEA BAKITA, WAKUBALIANA KUBIDHAISHA LUGHA YA KISWAHILI

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa akizungumza leo Oktoba 12,2023 alipotembelea Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), taasisi iliyopewa jukumu la kuendeleza Lugha ya Kiswahili duniani kote.

Katibu Mtendaji wa BAKITA, Consolata Mushi akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12, 2023 jijini Dar es Salaam, walipotembelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa. 
Katibu Mtendaji wa BAKITA, Consolata Mushi


Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI wamekubalina na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA kubidhaisha Kiswahili ili kiweze kuzungumzwa duniani kote.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa leo Oktoba 12,2023 alipotembelea Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), taasisi iliyopewa jukumu la kuendeleza Kiswahili duniani kote. Amesema kuwa Kiswahili kinawazungumzaji wengi watu zaidi ya milioni 200 wanazungumza lugha ya Kiswahili.

"Kama tuna watu zaidi ya milioni 500 wanzungumza Kiswahili maana yake, tunapo mahali pazuri pa kuanzia kuhakikisha tunabidhaisha Kiswahili chetu kinakwenda kwawatu zaidi ya milioni 500.

Kwahiyo tunalojukumu kubwa la kupeleka walimu wa Kiswaili katika nchi mbalimbali ambako wameomba kupata walimu wa Kiswahili, tutakaa na viongozi wa BAKITA na viongozi mbalimbali, tutashirikisha sekta binafsi tuhakikishe tunashirikiana kuhakikisha nchi mbalimbali ambazo zinataka kujifunza Kiswahili wanatumia walimu wa Kiswahili wa wakitanzania watakaokuwa na ujuzi na wanaojua kiswahili fasaha nasio viswahili vingine.", amesema Msigwa

Akizungumzia kuhusiana na wasio tumia Kiswahili fasaha, Msigwa amesema kuwa viswahili vya wajanja wajanja vinavyoharibu lugha ya Kiswahili watakuwa hawana nafasi kwani walimu watakaokuwa wakitakiwa ni wanaojua Kiswahili fasaha.

"Hatukatazi watu wengine kufundisha lakini tunataka Kiswahili kifundishwe kwa ufasaha wake." Ameeleza

Pia amesema kuwa watabidhaisha Kiswahili na kusimamia ubora wa Kiswahili katika nchi zote ambako tayari watu wanania ya kujifunza lugha hiyo.

Amesema kuwa Tanzania inamarafiki karibu nchi zote dunia hivyo hiyo ni fursa ya kupeleka Kiswahili katika nchi zote duniani, changamoto ni namna ya kuandaa walimu wa Kiswahili watakao kwenda kuungana na jitihada za kufundisha Kiswahili katika kila nchi, lakini kupanua wigo kwenye nchi ambazo hazijaanzisha madarasa ya kufundisha lugha ya Kiswahili.

"hatuna sababu ya kuharibu lugha yetu kwa sababu taasisi zinazofundisha kiswahili zipo nchini kwetu, BAKITA ipo nchini kwetu, wazungumzaji wazuri wa Kiswahili wapo Tanzania ni wengi kuliko mahali popote duniani." Amesema Msigwa

Amesema hakuna sababu ya Mtangazaji kwenda katika chumba cha habari na kutangaza kwa lugha isiyofasaha.

"Waandishi na Watangazaji, tuone fahari kuzungumza Kiswahili fasaha, sisi tukiona fahari na wengine wanaojifunza kiswahili wataona fahari kuzungumza kiswahili fasaha." Amesema

Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa BAKITA, Consolata Mushi amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa zakufundisha Kiswahili kwani Walimu wazuri na wenye weredi wa kufundisha Kiswahili wanatakiwa watoke Tanzania.

"Tanzania ni kinara wa Kiswahili wahiyo tunatumia fursa hiyo kuuza walimu wetu katika mataifa mbalimbali kwaajili ya kufundisha kiswahili na jambo hilo tumeshaanza kulitekeleza kwa sababu hata vyuo vikuu vilivyopo katika mfumo rasmi wameingia makubaliano na vyuo vikuu vingine katika kufundisha lugha ya Kiswahili.

Amesema kuwa hata vyuo visivyo na mfumo rasmi bado Watanzania wanatumika kufundisha Kiswahili kwa sababu wanaaminiwa na ndiyo wanaweza kufundisha lugha ya Kiswahili vizuri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad