HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 8, 2023

Kanisa la Halisi la Mungu Baba ya latoa Elimu katika Sherehe za Badiliko

*Baba Halisi anena kusudi la sherehe za Badiliko

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Kanisa la Mungu Baba limefanya Sherehe ya Badiliko ambayo inakwenda kutoa ufahamu kwa waumini na watanzania kwa ujumla.

Akizungumza katika Sherehe hizo ikiambatana na Ibada Kiongozi wa Kanisa hili Baba Halisi amesema kuwa kanisa hilo linasherehe tatu kwa mwaka ambapo sherehe ya Badiliko ni kufanya waumini kubadilika kujenga upendo na amani.

Baba Halisi amesema waumini kwa Kanisa hilo ndiyo chanzo kutaka dunia kuwa na amani na kikitokea kitu cha hatari kuomba kisitokee.

Amesema wakati sherehe hiyo ni kufanya waumini wabadilike hata katika maisha na changamoto za kila mmoja ziondoke na kuacha amani moyoni kwa waumini wa kanisa na taifa kwa ujumla.

Aidha Baba Halisi amesema  Taifa la Tanzania limebarikiwa kubarikiwa huko kunatokana na Mungu ndio aliyefanya kuwepo kubarikiwa kwa kuwa na amani iliyotukuka.

Amesema Baba Halisi chochote kinachoonekana ni kiwazo kiweze kuondoka  kwa waumini kwa uwezo wa Mungu Baba anayeombwa.

Mwakilishi wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam Mohamed Mbonde amesema hizo sherehe za Badiliko za Kanisa Halisi ziende kuondosha changamoto kwa waumini na watanzania kwa ujumla.

Mbonde amesema kuwa Kanisa Halisi la Mungu Baba limekuwa likifanya makubwa hivyo Baba Halisi abarikiwe kwa kutushirikisha.

Hata hivyo Baba Halisi katika ibada yake anasema juu ya amani na amani hiyo ndiyo inatawala katika nchi ya Tanzania.

Hata hivyo mmoja viongozi Moja Halisi amesema kuwa Baba Halisi amekuwa akiomba wakati wa majanga na kuondoka.

Aidha amesema kuwa mwaka huu katika mabadiliko ya Tabianchi juu ya Mvua za Elnino zitanyesha lakini madhara hayatatokea.

Kiongozi Moja Halisi wa Kanisa  la Halisi la Mungu Baba akizungumza kuhusiana na sherehe za Badiliko kwa Kanisa la Halisi la  Mungu Baba jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Mohamed Mbonde akitoa neno kwa niaba ya mkoa wa Dar es Salaam katika Sherehe za Badiliko katika Kanisa Halisi la Mungu Baba jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi akitoa mahubiri yaliyoambatana katika Ibada na Sherehe za Badiliko za Kanisa hilo  Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad