HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 5, 2023

Wakuu wa Vitengo na Wasimamizi wa Wodi Muhimbili wapigwa msasa

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Epvate & Fortune International Consultant Ltd wameendesha mafunzo kazi ya siku mbili kwa Wakuu wa Vitengo na Wasimamizi wa Wodi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kazi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Leila Komba amesema mafunzo haya ambayo yatafanyika kwa makundi tofati yataongeza weledi na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Tuyape umuhimu mafunzo haya kwani ulivyoingia sio kama utakavyotoka, sisi kama watendaji ndio injini ya hospitali hivyo tunakutana na wafanyakazi moja kwa moja,”amesema Bi. Komba.

Naye Bi. Upendo Mwansile ambaye ni msimamizi wa wodi tatu iliyopo Jengo la Mwaisela ameushukuru uongozi wa MNH kuandaa mafunzo hayo yatakayoongeza chachu ya utendaji.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utalawa Bi. Leila Komba.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Redemptha Matindi.
Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Ajira Bw. James Selega.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad