HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 31, 2023

FILAMU 234 ZIMEPITA KATIKA MCHUJO WA AWALI WA TUZO ZA FILAMU TANZANIA 2023

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa akizungumza na Wanahabari pamoja na Wadau wa Kazi za Sanaa Leo Oktoba 31,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa Kutangaza Filamu zilizofanikiwa kupita kwenye mchujo wa awali tuzo za Filamu 2023.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo akizungumza na Wanahabari Leo kutangaza Jumla ya Filamu 234 zimefanikiwa kupita kwenye mchujo wa awali wa tuzo za Filamu 2023 ambapo Kilele chake zinatarajiwa Kufanyika Disemba 2023, Ukumbi wa "The Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam
Wasanii mbalimbali wa Filamu waliojitokeza katika Mkutano wa kutangazwa rasmi kwa mchujo wa awali wa Filamu zilizoingia katika kinyang'anyiro cha Tuzo za Filamu 2023 Jijini Dar es Salaam

Na.Khadija Seif, Michuziblog
WASANII Waaswa Kutengeneza Kazi za Filamu zenye lengo la Kimkakati zenye maudhui ya kuitangaza nchi ili ziweze kuleta tija kwa Maslahi ya Taifa na nje ya mipaka ya Tanzania.

Akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 31,2023 Katika ukumbi wa Golden Tulip wakati akitangaza mchujo wa Filamu zilizoingia katika kinyang'anyiro cha Tuzo za Filamu 2023, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa ,Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa amesema mara nyingi watayarishaji na wasanii wa Filamu wamekuwa wakitengeneza kazi zenye mahitaji na kulenga hadhira fulani pasipo kugundua kuwa kwenye jamii kuna matukio mengi hususani matukio ya Kimkakati katika Sekta mbalimbali ikiwemo ya Utalii,Uchumi ambapo kwa kupitia kazi za filamu zinatakiwa kufikisha ujumbe nje na mipaka ya Tanzania .

"Sina maana kuwa kazi mnazofanya sio sahihi hapana lakini kuna namna amabpo tunatakiwa tuangalie matukio katika jamii yetu ambayo yanatakiwa kumulikwa na kuonekana kwenye kazi za filamu ili ziweze kuleta tija zaidi Rais wetu Dkt.Samia Suluhu ameiona fursa kupitia filamu "The Royal Tour " na sisi tuendelee alipoishia kwa kuingia kwake kwenye hii tasnia ametuheshimisha sana na sisi tusibaki nyuma tutengeneze kazi zenye tija na kuimarisha uchumi na pato la taifa.

Hata hivyo Msigwa amesema Bodi ya Filamu imepiga hatua kubwa kwa kuendeleza tuzo hizo zenye kuleta hamasa kwa wasanii kutengeneza kazi nyingi zenye ubora zaidi huku akitoa maagizo kwa taasisi zilizo chini ya Wizara Kuhakikisha sekta ya burudani inavutia wadhamini kwa kiasi kikubwa.

"Uwepo wa wadhamini mbalimbali wanaotoa ushirikiano kwenye matamasha ya Sanaa ni nguvu tosha na nia ya dhati kuona tuzo hizi zinahitajika kuendelezwa mwaka hadi mwaka kwa kutumia nguvu,maarifa ikiwemo pesa za wadhamini hao hivyo Taasisi zilizopo chini yangu zinatakiwa zitekeleze majukumu ya kuhakikisha wadhamini wanapata nafasi ya kujitangaza vizuri ."

Pia ametoa rai kwa wasanii kuhakikisha wanajisajili bodi ya filamu ili waweze kunufaika na kutambulika na kazi zao za Sanaa ikiwemo kupata nafasi ya kukopesheka fedha katika Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa.

Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo amesema Mchakato wa tuzo ulizinduliwa mapema Agosti na kuwapa nafasi wasanii kuwasilisha kazi zao ambapo kwa msimu wa tatu kipengele cha kujipendekeza kimeondolewa kutokana na maoni ya majaji kuona hakiwezi kukidhi kwa jicho la jopo la majaji.

Dkt.Kilonzo amesema idadi ya Filamu zilizopita mchujo wa awali ni kubwa zaidi kulinganisha na miaka ya nyuma. Mwaka Jana jumla ya Filamu 189 zilipita mchujo kati ya Filamu 840 zilizopokelewa.

"Mwaka huu jumla ya Filamu 204 zimekidhi vigezo katika hatua hii ya awali, kati ya Filamu 565 zilizokusanywa. Kitakwimu, mwaka huu 41% ya Filamu zilizokusanywa zimekidhi vigezo, ikiwa ni ongezeko la 18% kutoka 23% ya Filamu zilizochaguliwa mwaka jana."

Pia ameeleza kuwa Kufuatia zoezi la ukusanyaji wa Filamu kutoka Mikoa ya Tanzania Bara, Zanzibar na Nchi za Afrika Mashariki, Bodi ya Filamu imetangaza jumla ya Filamu 234 zilizopita katika mchujo wa awali wa Tuzo za Filamu Tanzania 2023, katika hafla iliyofanyika Oktoba 31 jijini Dar es Salaam

"Jumla ya Filamu 565 zilipokelewa kwa nia ya kushiriki katika vipengele vya Tuzo za mwaka 2023 ambapo Filamu 535 zimetoka Tanzania na Filamu 30 kutoka nje ya Tanzania katika Nchi za Kenya, Uganda na DRC."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad