HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 1, 2023

Benki ya NBC, Wachezaji Azam FC, Twiga Stars Waendesha Kliniki ya Michezo kwa Watoto

 

[Dar es Salaam: Septemba 30, 2023] Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) , mdhamini Mkuu wa Ligi ya Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premiere League) imeendesha program yake ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kukuza mchezo wa soka hapa nchini.
Katika kufanikisha program hiyo iliyofanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, benki hiyo ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wazazi na watoto wao walioungana na baadhi ya wachezaji vinara kutoka klabu ya soka ya Azam FC wakiwemo Prince Dube, Abdul Suleiman 'Sopu', Lusajo Mwaikenda na Iddi Selemani Nado.

Pia walikuwepo baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Stumai Abdallah na Fatuma Issa. Kupitia program hiyo benki hiyo pia ilikabidhi mipira 30 kwa Academy ya vijana ya Magnet ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za taasisi hiyo kulea kuendeleza vipaji vya michezo hapa nchini.

Akizungumzia programu hiyo Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo alisema ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kukuza mchezo huo sambamba na kuchochea kasi ya ajira nchini kupitia sekta ya michezo.

”Mkakati wa benki ya NBC kwasasa ni kuhakikisha sekta ya michezo inageuka kuwa ajira. Katika kufanikisha hili tulianza na udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, tukaona pekee haitoshi tukaongeza udhamini wetu hadi kwenye Champion League na sasa kupitia program yetu hii ya NBC Chanua Account Football Clinic tunalenga kuibua vipaji chipukizi kabisa vya mchezo huu pendwa. ‘’

‘’Katika kufanikisha hili pamoja na kuandaa program za mazoezi kwa watoto tutakuwa pia tunawakutanisha na wachezaji vinara hapa nchini ili waweze kuwapa hamasa chipukizi hawa waongeze juhudi kwenye michezo huku pia wakiwapa mbinu mbalimbali za kimichezo,’’ alifafanua.

Kwa mujibu wa Alina, kupitia program hiyo inayotarajiwa kufanyika angalau mara nne kwa mwaka, walengwa ambao ni watoto wenye umri kuanzia miaka sita hadi kumi na tatu pia watapata fursa ya kupewa elimu kuhusu fedha hususani umuhimu wa kujiwekea akiba huku wazazi pia wakipata fursa ya kupewa elimu kuhusu malezi ya watoto hasa kwenye masuala yanayohusiana na ulaji wa vyakula sahihi, umuhimu wa mazoezi, mabadiliko ya kiukuaji kwa watoto na namna ya kutambua vipaji vya watoto wao.

Wakizungumzia hatua hiyo wachezaji walioshiriki programu hiyo, pamoja na kuipongeza benki ya NBC kwa jitihada zake katika kuendeleza mchezo wa soka hapa nchini, walionyesha kufurahishwa zaidi na mpango huo kwa kuwa unatoa fursa kwao kushirikiana na jamii hususani watoto, hatua ambayo itasaidia sana kuwashawishi wazidi kuupenda mchezo huo sambamba na kuongeza juhudi zaidi waweze kufanikisha ndoto zao kupitia michezo.

‘’Imekuwa ni furaha sana kwetu hii leo na kwa hili tunawapongeza sana NBC kwa kuwa kupitia program hii ya NBC Chanua Account Football Clinic wametukutanisha na watoto ambao tumeweza kucheza nao, tumewaelekeza baadhi ya mbinu chache za kimichezo na zaidi tumewahamasisha waendelee kupenda michezo sambamba na kuzingatia masomo yao kwa kuwa elimu na michezo vinaweza kabisa sambamba.’’

‘’Zaidi kwa kuwa program hii inahusisha wazazi tunaamini kabisa itasaidia kubadili mitazamo yao kuhusu suala zima la kuheshimu vipaji vya watoto wao,’’ alisema mchezaji Sopu, mshambuliaji wa timu ya Azam FC.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi walioshiriki tukio hilo wakiwa sambamba na watoto wao walisema wamevutiwa zaidi na program ya NBC Chanua Account Football Clinic kwa kuwa imehusisha maeneo mengi muhimu yenye manufaa kwa watoto ikiwemo michezo, elimu ya fedha na akiba, afya na malezi ya watoto huku pia ikitoa fursa kwa wazazi na watoto kufurahia pamoja sambamba na wachezaji wanaowapenda kutoka Ligi Kuu ya NBC.

Baadhi ya wachezaji wa Azam FC Abdul Suleiman 'Sopu', Lusajo Mwaikenda na Iddi Selemani Nado pamoja na mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Stumai Abdallah, wakimfuatilia mshambualiaji wa Azam FC Prince Dube wakati akielekeza mbinu mbalimbali za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto walioshiriki program mpya ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayoratibiwa na Benki ya NBC, inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Programu hiyo ilifanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Anaeshuhudia pia ni Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo (alievaa kofia)

Baadhi ya wachezaji wa Azam FC Abdul Suleiman 'Sopu', mshambualiaji wa Azam FC Prince Dube na Iddi Selemani Nado pamoja na mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Stumai Abdallah, wakimfuatilia mchezaji wa Azam FC Lusajo Mwaikenda wakati akielekeza mbinu mbalimbali za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto walioshirikiprogram mpya ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayoratibiwa na Benki ya NBC, inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Programu hiyo ilifanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Anaeshuhudia pia ni Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo (alievaa kofia)Baadhi ya wachezaji wa watoto na wazazi wakimfuatilia mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Stumai Abdallah, wakati akielekeza mbinu mbalimbali za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto hao walioshiriki program mpya ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayoratibiwa na Benki ya NBC, inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Programu hiyo ilifanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Fatuma Issa (Kushoto) akishiriki michezo na watoto walioshiriki program mpya ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayoratibiwa na Benki ya NBC, inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Programu hiyo ilifanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wachezaji wa Azam FC Abdul Suleiman 'Sopu', Lusajo Mwaikenda na Iddi Selemani Nado na Prince Dube pamoja na mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Stumai Abdallah (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja baadhi ya maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo (kushoto) pamoja na watoto walioshiriki program mpya ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayoratibiwa na Benki ya NBC, inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Programu hiyo ilifanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo (alievaa kofia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kocha wa Academy ya vijana ya Magnet Ramadhani Hussein (wan ne kushoto) sambamba na watoto ambao ni wachezaji wa klabu hiyo mara baada ya benki hiyo kukabidhi mipira 30 kwa Academy hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za taasisi hiyo kulea kuendeleza vipaji vya michezo hapa nchini. Tukio la makabidhiano hayo lilifanyika wakati wa uzinduzi wa program mpya ya michezo kwa watoto inayofahamika kama NBC Chanua Account Football Clinic inayoratibiwa na Benki ya NBC, inayolenga kuibua vipaji vya watoto wadogo. Programu hiyo ilifanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.




Katika kufanikisha program hiyo iliyofanyika viwanja vya Agha Khan, eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, benki hiyo ilihusisha wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wazazi na watoto wao walioungana na baadhi ya wachezaji vinara kutoka klabu ya soka ya Azam FC wakiwemo Prince Dube, Abdul Suleiman 'Sopu', Lusajo Mwaikenda na Iddi Selemani Nado. Pia walikuwepo baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Stumai Abdallah na Fatuma Issa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad