HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 28, 2023

CMSA yatunuku vyeti, tuzo

 

 Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeeleza kuwa ina jukumu la kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa na faida zinazopatikana katika masoko ya mitaji na kujenga uwezo wa wataalamu wanaotoa huduma katika kada hiyo.


Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, CPA Nicodemus Mkama, akizunguma katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la masoko ya mitaji kutoka vyuo vikuu jijini Dar es Salaam, amesema utoaji wa elimu ya fedha kwa umma na kujenga uwezo wa wataalam wanaokidhi viwango vya kimataifa ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha,(Financial Sector Development Master Plan 2019/20 – 2029/30.

Amesema mpango huo wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu.

Mkama amesema CMSA, iliendesha Shindano kwa Wanafunzi wa Vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu, kuhusu uelewa, ueledi wa masoko ya mitaji na uwekezaji wa pamoja kwa kutumia njia ya mitandao ya kielektroniki yaani simu za mikononi na intaneti.

Amesema shindano hilo limeweza kuvutia Mamlaka za Masoko ya Mitaji za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuja nchini kujifunza jinsi ya kuendesha mashindano kama haya katika nchi zao kwa kutumia simu za mkononi na intaneti.

Aidha amesema mamlaka hiyo imeweka mpango wa kuwawezesha washiriki wa shindano kuwa wawekezaji halisi.

Katik jitihada za kuongeza idadi, ueledi na ufanisi wa wataalamu wa masoko ya mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa wenye lengo la kukuza na kuendeleza masoko ya mitaji hapa nchini, Mamlaka inashirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Uwekezaji na Dhamana (CISI) ya nchini Uingereza, kuendesha mafunzo yanayotambulika kimataifa,”amesema.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanajenga uwezo na ufanisi kwa watendaji wa masoko ya mitaji pamoja na ujuzi kwa wahitimu unaowawezesha kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ya sekta ya masoko ya mitaji na dhamana ulimwenguni.

Washindi wa shindano la CMSA,wakikabidhiwa  mfano wa hundi ya fedha ikiwa ni sehemu ya zawadi zilizotolewa na mamlaka hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Fedha, akimtunuku cheti cha kozi ya watendaji wa masoko ya mitaji mmoja wa wahitimu wanaokidhi viwango vya kimataifa , anayeshuhudia kushoto ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama.
Picha ya pamoja baina ya Viongozi na washikiri wa kozi ya watendaji katika masoko ya mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa.
Kutoka kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama, wa pili ni Naibu Waziri wa Fedha,Hamad Hassan Chande, mmoja wa mhitimu mwenye shahada ya juu ya uzamivu aliyekabidhiwa cheti cha wtendaji wa juu wanaokidhi viwango vya kimataifa, wa mwisho ni Mwenyekiti wa Bodi ya CMSA,Dk. John Mduma.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa CMSA,sekta za fedha na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa shidano la Taasisi za elimu ya juu na vyeti kwa wahitimu wa kozi za watendaji katika masoko ya mitaji.
.Afisa Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) ,CPA.Nicodemus Mkama, akifurahia ahadi ya ushirikiano iliyotolewa na Prof. Mohamed Warsame,  wakati wa utoaji zawadi kwa washindi wa shindano la CMSA kwa Taasisi za Elimu ya Juu.
Profesa Mohamed Warsame akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mipango,Ofisi ya Umoja wa Ulaya (EU),Bi Mihaela Marcu.

Majaji wa shindano la Taasisi za Elimu ya juu wakisikiliza kwa makini majibu ya maswali ya washiriki.
Baadhi ya Watendaji ya Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana wakishuhudia utoaji wa tuzo na vyeti.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad