HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 4, 2023

WANACHAMA DLCO-EA KUFANYA MAGEUZI, KUWA NA NGUVU YA PAMOJA KUDHIBITI VISUMBUGU MAZAO

 

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza leo Septemba 4, 2023 wakati wa mkutano wa shirika la kudhibiti nzige wa jangwani Mashariki mwa Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza leo Septemba 4, 2023 wakati wa mkutano wa shirika la kudhibiti nzige wa jangwani Mashariki mwa Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam.





Matukio mbalimbali.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KUELEKEA Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) wanachama wa shirika la kudhibiti Nzige wa jangwani Mashariki mwa Afrika (DLCO-EA) wakutana kujadili nini kifanyike ili kuongezea nguvu kwaajili ya kupambana na visumbufu mazao katika nchi tisa za Mashariki mwa Afrika.

Wanachama wa shirika hilo ni nchi tisa ambazo ni Tanzania ambao ndio mwenyeji wa mkutano, Uganda, Kenya, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djbouti, Sudani na Sudani Kusini.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Septemba 4, 2023 amesema kuwa wametumia mkutano wa AGRF ili kufanya mkutano mkuu wa DLCO-EA nakukubaliana kufanya mageuzi ya shirika hilo ili kuwa na nguvu za pamoja kupambana na Viumbe wa haribifu kabla hawajaleta madhara makubwa ya mazao.

Bashe amesema wamekubaliana kwamba kila nchi iwekeze rasilimali ziweze kuwahusisha na kusaidia nchi mwanachama ikitegemea na hali gani ya kiuchumi na wadudu wanaweza kutoka nchi jilani na kuathiri nchi nyingine.

Amesema ni nchi mwanachama watashirikiana kwenye rasilimali zitakazo kuwepo.

Akizungumzia mafanikio ya shirika hilo, Waziri Bashe amesema mafanikio ni makubwa kwani 2021 Tanzania, Kenya, Ethiopia, Somalia na Uganda Kidogo zilishambuliwa na viumbe waharibifu wa mazao na wakadhibitiwa kabla haijaletwa madhara makubwa.

Amesema kuwa wamepanga kufanya tafiti ambazo zitakuwa zinatoa taarifa mapema kabla ya wadudu waharibifu hawajaharibu mazao shambani.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimagu amesema kuwa mkutano wa 68 wa baraza la Uongozi la mawaziri wa shirika la kudhibiti nzige jangwani Mashariki mwa Afrika.

Amesema shirika hilo wanashirikiana katika kuchangia rasilimali mbalimbali ili kuhakikisha kwamba nzige wanateketezwa kwa kutumia ndege nyuki zisizo na rubani (drone) kwaajili ya kunyunyizia viwatilifu.

Amesema kutokana na majukumu ya shirika hilo ya kudhibiti nzige wa jangwani lakini kwa sasa wameanza kudhibiti visumbufu vingine vya mazao kama kwelea kwelea ambao wanaweza kuharibu mazao ya nafaka kwa asilimia 100.

Viumbe hao waharibifu ni Viwavijeshi, Nzige, Mbugo na ndege aina ya Kweleakwelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad