NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA
la Viwango Tanzania (TBS), limeshiriki Bonanza la Michezo kwa
wafanyakazi wa shirika hilo lengo likiwa ni kuwakutanisha pamoja
watumishi katika michezo ili kuboresha afya na kujenga mahusiano mazuri.
Akizungumza
hapo jana Septemba 2,2023 katika Bonanza hilo ambalo limefanyika kwenye
viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya TBS,
Prof.Othuman Chande amewapongeza wanaviwango waliojitokeza kushiriki
pamoja na kushangilia katika kipindi chote cha bonanza.
“Hii
itasaidia kuboresha afya zao na kujenga mahusiano mazuri kati ya
watumishi, kwani utekelezaji mzuri wa majukumu yenu ya kila siku
hutegemea sana afya ya mwili na akili”. Amesema
Amesema watumishi
na watoa huduma wa Shirika la Viwango Tanzania wameshiriki katika
michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa Pete, mpira wa
wavu, kuvuta kamba na michezo ya jadi ambapo mashindano haya
yameshindanishwa kiidara.
“Vilevile kupitia michezo hii watumishi
hupata burudani na hupunguza msongo wa mawazo unaoweza kusababishwa na
kukosa nafasi ya kufanya mazoezi au kushiriki michezo mbalimbali”.
Amesema
Sunday, September 3, 2023
Home
Unlabelled
VIWANGO SPORTS BONANZA YAWAKUTANISHA PAMOJA WATUMISHI WA TBS
VIWANGO SPORTS BONANZA YAWAKUTANISHA PAMOJA WATUMISHI WA TBS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment