HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 27, 2023

TUNZAA YATANGAZA USHIRIANO NA VODACOM KUPITIA M-PESA, AFRIKA KUFIKIWA NA HUDUMA

Meneja Malipo ya Kidijitali na Chaneli za Mtandaoni kutoka Vodacom Tanzania, Josephine Mushi (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutambulisha ushirikiano na kampuni ya Kiteknolojia ya Tunzaa. Ushirikiano huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2023. 

Mkuu wa idara ya huduma kwa wateja Tunzaa,Abdallah Said akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2023 wakati wa kutambulisha ushirikiano na Kampuni ya Vodacom Kupitia M-Pesa.
Mkurugenzi mtendaji - Tunzaa Ng'winula Kingamkono akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2023.

*Wateja wa Vodacom Kuanza Kutumia aplikesheni ya Tunzaa ndani ya aplikesheni ya M-Pesa

KAMPUNI ya Kitanzania ya teknolojia ya Tunzaa ambayo imejikita katika kutatua changamoto za tabia za kifedha kwa Waafrika kwa kutumia teknolojia leo Septemba 27, 2027 wameanza kushirikia na kampuni ya Vodacom kupitia M-Pesa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Tunzaa, Abdallah Saidi amesema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuimarisha tabia chanya za kifedha kwa Waafrika wa kila siku kwa kuwawezesha kununua bidhaa kwa njia ya awamu bila madeni.

“Ushirikiano huu unaashiria hatua katika biashara za kimtandao kwani Tunzaa kwa kushirikiana na M-Pesa tunatoa suluhisho rahisi la manunuzi ya kimtandao na kuongeza uhuru wa kifedha kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla na lengo la jukwaa hili ni kuwawezesha Waafrika wa kawaida kwa kupata njia salama, bora, na endelevu ya kupata bidhaa na huduma wanazohitaji.”

Amesema Tunzaa inatoa huduma zake Tanzania nzima na hapo baadae ina lengo la kutanua wigo kufikia nchi za jirani kama Kenya, Uganda, Kongo, Zambia, Malawi, Msumbiji na baadae kufikia nchi zote za Kiafrika.

Akizungumzia kuhusu wateja wake, amesema Tunzaa imeshahudumia watu zaidi ya 25,000 ambao wamejisajili kwenye jukwaa hilo na imewezesha mamia ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao kupitia Jukwaa la hilo.

“Watumiaji wa Tunzaa wanalipia bidhaa kidogo kidogo yaani Tunza Sasa, Nunua baadae yaani kwa kudunduliza kwa kipindi cha hadi miezi sita kwa bidhaaa yoyote atakayoichagua.” Amesema Saidi

Akizungmzia kuhusiana na bidhaa ambazo mteja anaweza kununua kwa kudunduliza ametaja kuwa ni vifaa vya nyumbani, Runinga, mashine za kufulia, majokofu, simu za mkononi, na vifaa vingine.

“Kuanzia leo wateja wote wa Vodacom wanaotumia huduma ya M-Pesa kwa ajili ya kufanya mihamala yao wataweza kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa kulipa kidogo kidogo kutoka kwenye aplikesheni ya Tunzaa itakayokuwa ndani ya aplikesheni ya M-Pesa moja kwa moja.”

Pia amesema kuwa Huduma zote za Tunzaa sasa zitafanyika ndani ya aplikesheni ya M-Pesa, hatua ambayo itasaidia watumiaji wa M-Pesa kuweza kufanya miamala na kununua bidhaa wakiwa wanaendelea na huduma nyingine za M-Pesa.

Kwa Upande wa Meneja Malipo ya Kidijitali na Chaneli za Mtandaoni kutoka Vodacom Tanzania Josephine Mushi, amesema kuwa kuanzia leo Tunzaa inapatikana ndani ya M-Pesa super App hii inawarahisishia wateja wetu kufanya manunuzi ya bidhaa wanazohitaji kwa kulipia kidogo kidogo, sasa wateja wa M-Pesa wanaweza kuwekeza fedha zao huku wakinunua bidhaa.

“Sasa watumiaji wa App ya M-Pesa wanaweza kununua bidhaa wanazopenda kupitia App ya Tunzaa iliyopo ndani ya M-Pesa, hivyo manunuzi yatakuwa rahisi sana bila usumbufu wowote" Ameeleza

Mkurugenzi mtendaji Tunzaa, Ng'winula Kingamkono amestoa rai kwa serikali kuongeza vituo vya ufundishaji wa teknolojia viwepo kwenye kila chuo kikuu, ili vijana waweze kujifunza vizuri teknolojia na kuweza kuleta maendeleo nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad