HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 25, 2023

TAMASHA LA TDF KUBAMBA GEITA NOVEMBA, WANAFAGDI NI 'DOOR TO DOOR'

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza leo Septemba 25, 2023 jijini Dar Es Salaam Katika Mkutano na waandishi wa habari Kuelekea Utekelezaji wa Tamasha la Maendeleo, (Tanzania Development Festival).

Na Mwandishi wetu.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa jukumu la kuzuia vitendo vya ukatili ni la kila mwanajamii na kila taasisi hapa nchini ili kufikia fursa za kiuchumi.

Ameyasema hayo leo Septemba 25, 2023 wakati wa kutambulisha rasmi siku ya kufanyika tamasha la huduma za kutangaza Maendeleo (Tanzania Development Festival (TDF) litakalofanyika katika mikoa 16 kwa awamu ya kwanza kwa Mwaka huu.

Tamasha hilo kwa Mikoa hiyo 16 litaanzia katika Mkoa wa Geita kuanzia Novemba 1-5, 2023. Likiwa na Kauli Mbiu; "Zijue Fursa, Imarisha Uchumi, Kataa Ukatili Kazi Iendelee"

Mikoa mingine itakayofikiwa kwa awamu ya kwanza ni Shinyanga, Morogoro, Dodoma, Arusha, Manyara, Pwani, Mwanza, Kagera, Mbeya, Kigoma, Mara, Sogwe, Tanga, Ruvuma na Tabora.

Amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau iliingia mkataba wa kisheria (MOU) na Taasisi ya Foundation For Ambassadors Gender Development Initiatives (FAGDI) ambao ni wasanii mbalimbali na watu maarufu katika jamii mbalimbali ili wawe mabalozi wa kutekeleza kampeni ya ZIFIUKUKI (Zijue Fursa Imarisha Uchumi Kataa Ukatili Kazi Indelee) kupitia matamasha hilo.

Katika kuendelea kuelimisha jamii kupinga ukatili na kufikia fursa za kiuchumi ili kutokomeza umaskini ambapo pia huchochea ukatili Waziri Dkt. Doroth amewaomba viongozi wa mikoa ambapo tamasha la DTDFlitafanyika kuipokea timu ya waratibu na kuipa ushirikiano ili kutimiza malengo yake.

Pia amewaomba Wadau mbalimbali wanaofanya kazi na Wizara kushirikiana kubeba ajenda ya kuhamasisha, kutoa huduma na kuelimisha jamii ifahamu na kutambua fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia Tanzania Development Festival Kampeni ya ‘ZIFIUKUKI’.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Taasisi ya Foundation For Ambassadors Gender Development Initiatives (FAGDI), Simon Mwapagata amesema kuwa Tamasha hili litakalofanyika Mkoani Geita ushiriki wa wananchi utakuwa ni mkubwa kwani kila balozi wa FAGDI atakuwa na nafasi ya kuzungumza na washiriki kwa njia mbalimbali.

"Njia itakayotumika ni Door to Door pia wasanii watageuka kuwa baraka kwa watoto katika kutoa elimu ya kuzuia ukatili wa watoto na jamii kwa ujumla." Amesema Mwapagatwa

"Shukrani zangu ziende kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, kwa kujitoa kwake kuhakikisha fursa hii inawafikia wana Geita. Aidha, shukrani kwa Waratibu wa Wizara na Taasisi ya FAGDI ambao ni Mabalozi wa kuhamasisha masuala ya uwezeshaji wanawake kiuchumi na kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto." Amesema Dkt. Doroth

Pia ametoa Shukrani kwa watu wote waliolishiriki wakiwemo Mabalozi wa Wizara na Wadau mbalimbali wa Maendeleo kwa kujitolea kubeba ajenda hii ya kitaifa ya kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya fursa za kiuchumi, mapambano dhidi ya ukatili na kuelimisha jamii ya juu ya kulinda maadili, mila na desturi zetu.

"Wito kwa maafisa maendeleo na maafisa ustawi wa jamii, Wadau wote kushiriki kikamilifu katika kuratibu Kampeni hii katika Mikoa yao kujitokeza kwa wingi kushiriki katika jukwaa hili la pamoja ili kuelimisha wananchi juu ya fursa za kiuchumi." Amesema

Tamasha la TDF lilizinduliwa Aprili 27-29, 2023, Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Sekta Binafsi ambao walitoa huduma, taarifa, elimu na maonesho kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi bila malipo zikiwemo huduma za kibenki, afya, msaada wa kisheria na bima.

Takribani watu 16,000 walihudhuria na kati yao watu 4040 walipata huduma ndani ya siku mbili tu.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Taasisi ya Foundation For Ambassadors Gender Development Initiatives (FAGDI), Simon Mwapagata akizungumza leo Septemba 25, 2023 jijini Dar Es Salaam Katika Mkutano na waandishi wa habari Kuelekea Utekelezaji wa Tamasha la Maendeleo, (Tanzania Development Festival).Matukio mbalimbali. wakionesha Mabango kupinga Ukatili katika Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad