HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 23, 2023

TMDA YATOA MWITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA MADHARA YA DAWA

 

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba( TMDA) Adam Fimbo ametoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa za madhara yanayotokana na dawa pindi wanapokutana na changamoto hiyo ili waichukue dawa hiyo sokoni na kuifanyia vipimo ili kuokoa wengine.
Fimbo ametoa mwito huo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Kikao kazi cha Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali nchini kuelezea mafanikio waliofanya kwa miaka 20 ya TMDA na kutambua mchango wa vyombo vya Habari katika kuelimisha umma.

Akieleza zaidi amesema dawa zinazotumika kutibu magonjwa mbalimbali zinaweza zikatibu au zisitibu na kuleta madhara kwa mtumiaji, hivyo mwito wao kwa wananchi ni wao ndio wanatumia kila siku kwa ugonjwa ambao unakusumbua.

"Hivyo tunaomba utoe taarifa ukiona dawa fulani inakusumbua au unatumia haikupi matakoe ambayo yanatakiwa,”amesema Fimbo.

Ameongeza TMDA ina mifumo inayosaidia wao kufahamu dawa kama inatibu au haitibu lakini kutokana na asili ya dawa hizi ni kemikali zikikaa muda fulani au kutegemeana na mwili wa binadamu uko dhaifu kiasi kiasi gani.

Pia amesema usajili wa dawa unasaidia kuhakiki au kudhibiti kwa sababu matoleo yanatengenezwa katika vipindi tofauti inawezekana ikatokea dawa ina shida fulani.

Fimbo amesema dawa jinsi zilivyo zina madhara kwa watumiaji hivyo amesisitiza kwa wananchi kama dawa anayotumia inaleta madhara atoe taarifa ili kufahamu dawa ina madhara kwa watu wa aina gani wazee, watoto wajawazito ili itusaidie kubaini madhara mapema na kuweza kuchukua hatua mapema ili athiri isitokee kwa walio wengi.

" Hili ni jukumu kubwa la TMDA kwani kuna dawa bandia na duni sokoni kwa sababu dawa hazina mipaka zinavuka ikitokea dawa una mashaka nayo unapaswa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika."

Akieleza zaidi amesema pia TMDA inaongoza barani Afrika katika suala la mifumo na udhibiti wa dawa ukaguzi wa usajili, bidhaa na usalama wa dawa kwenye soko.

Amesema mifumo yote imefanyiwa uhakiki na Shirika la Afya Duniani (WHO) sasa hivi wanaongoza na wenzao wa SADEC wamekuja kujifunza taratibu ziko je na tunafanya je kazi na tunatoa mafunzo, “amesema.


Pamoja na hayo amesema kushirikiana na waandishi wa habari na wahariri wameona umuhimu kwa kazi wanazofanya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu TMDA na kulinda afya za jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mdhibiti wa Dawa Vifaa Tiba na Vitendanishi wa TMDA Kissa Mwamita ametoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili wao wakaelimishe jamii.

Ameongeza kuwa madhara yatokanayo na vifaa vya afya kuna mifumo ambayo mwananchi akitumia dawa au vitendanishi watoe taarifa TMDA ili waweze kufanya tathimini.

Pia amesema kupatikana kwa madhara pia kuna sababishwa na hali tofauti inawezekana ikawa ni ugonjwa au mchanganyiko na dawa nyingine.

Wakati huo hu Mkurugenzi Huduma ya Maabara TMDA, Dk. Dastan Hipolite ameeleza kwamba maabara ya mamlaka imeendelea kupokea sampuli ambapo mpaka sasa wamepokea sampuli 1372 za dawa kwa mwaka tangu 2006 hadi 2023.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika maabara ikiwemo vifaa vya kisasa vya upimaji sampuli mashine na mpaka nchi za jirani wanakuja kujifunza hapa na kuleta sampuli zao TMDA.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Bw. Adam Fimbo akizungumza na vuombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania kuhusu maadhimisho ya miaka 20 na mafanikio ya taasisi hiyo Leo jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)



Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Gaudencia Simwanza akiwasilisha mada ya Wajibu wa Waandishi wa Habari katika kulinda Afya ya Jamii, katika kikao kazi cha TMDA na Waandishi wa Habari,Septemba 22.2023.





Kaimu Mkurugenzi wa dawa za binadamu na mifugo , Emmanuel Alphonce akiwasilisha mada kwa Waandishi wa Habari waliohudhulia katika kikao kazi hicho,Septemba 22.2023.






























No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad