HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 29, 2023

MWALIMU AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUWAINGIZA VIDOLE SEHEMU ZA SIRI WATOTO WATANO

 

Njombe
MWALIMU wa kiume aliyejulikana kwa jina moja la Ngoitanile anayekaribia kuwa na umri wa miaka stini (60) anayefundisha katika shule ya msingi Mwembetogwa iliyopo Mtila kata ya Matola halmashauri ya mji wa Njombe,amekamatwa na polisi kwa tuhuma za ukatili wa kuwaingiza vidole sehemu za siri watoto watano wanaosoma darasa la kwanza na la tatu na kuharibu usichana wao.

Kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa Njombe ambaye pia ni kaimu kamanda Butusyo Mwambelo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa mara baada ya kupata taarifa za uficho na kwenda kumkamata mwalimu huyo.

"Bahati nzuri tulikuwa na majina ya wale watoto ambao wako watano, wawili ni darasa la kwanza na watatu ni wa darasa la tatu kwa hiyo tukafanya utaratibu wa kuwapeleka hospitali na dakatari akatoa taarifa kwamba hao watoto inaonekana sehemu zao za siri wameingiliwa na kitu butu hawana bikira"amesema kamanda Mwambelo

Amesema mara baada ya taarifa hizo walilazimika kuwahoji watoto hao juu ya vitendo walivyofanyiwa ambapo waliweka wazi kuwa wamekuwa wakiingizwa vidole sehemu za siri na mwalimu huyo wakiwa darasani huku wakati mwingine akiwaita ofisini.

"Kibaya zaidi walipoulizwa wanafunzi wengine nao wakikiri kweli kwamba huyu babu anafanya hicho kitendo mbele ya wanafunzi na lile darasa kuna watoto wa kiume na watoto wa kike,kwa hiyo huyu mwalimu yupo hapa kituo cha polisi lakini ushirikiano kwa walimu tumekosa wamesema hizo taarifa hawana ila watoto ndio wamesema"ameongeza Kamanda

Kamanda Butusio ametoa wito kwa wanannchi wa mkoa wa Njombe kuacha kuficha taarifa za matukio kama hayo na kutoa ushirikiano kwa polisi huku pia akibainisha kuwa kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi ya mtuhumiwa na hakuna dhamana itakayotolewa kwake kwa sasa mpaka Mahakamani lakini sio kwa jeshi la polisi.

2 comments:

  1. Mwalim huo Hana akili afungwe apate hakili Hana mwanamke wakufanyia hivo asiachiwe kwanza huo

    ReplyDelete
  2. mhhhhh!! matatizo mengine yakujitakia kama ndo kweli we mwalim wewe wanawake woote hao waliojaa hata wajane ?? ila tu kwa umri tajwa hapo juu basi vyombo vya usalama fanyeni kwanza upelelezi wa kutosha ikiwa kama nisehemu yenu ya kazi na pia mwalimu nae apelekwe akapimwe akili ili kujiridhisha kama yupo sawa kiakili🙏🙏

    ReplyDelete

Post Bottom Ad