HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 21, 2023

MJUMBE HALMASHAURI KUU CCM ACHANGIA KUDHIBITI TEMBO WANAOVAMIA MAKAZI YA WATU

 



Na Mwandishi Wetu, Simiyu
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa kutoka Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu Silanga amechangia kiasi cha Shilingi Milioni mbili kwa ajili ya kununua pikipiki zitakazotumika kuongeza nguvu ya kudhibiti tembo wanaovamia makazi ya Wananchi Wilayani Meatu Mkoani humo.

Mbali na kuchangia kiasi hicho cha fedha, pia Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ametoa zaidi ya Shilingi Milioni 2 za kununua saruji kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Chama katika Kata ya Mwasengela Wilayani Meatu na Kata

Ikindilo Wilayani Itilima, sambamba na kuchangia shilingi milioni tatu za ujenzi wa nyumba ya mtumishi UWT wilaya ya Itilima na milioni moja kwa ajili ya nyumba ya Mtumishi wa UWT wilaya ya Maswa.

Akizungumza na Wananchi wa Kata hizo pamoja na viongozi wa Chama na Serikali akiwa ameambatana na Mjumbe wa Halmashauriu Kuu Taifa kupitia Umoja wa Wanawake UWT, Nadra Gulam, wakiwa katika ziara ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Taifa, Mary Pius Chatanda, Gungu amesema viongozi lazima wawe mstari wa Mbele kuonyesha mfano wa kudhibiti tembo kwa kusaidia vifaa vya kukabiliana nao ikiwemo pikipiki ambazo zitatumiwa na askari kuwafukuza tembo Hao.

"Unajua lazima sisi viongozi tuwe mfano katika kukabiliana na suala la tembo hapa Meatu. Rais Dk Samia amefanya mengi, amejenga vituo vya askari wa wanyamapori, ili kuwaleta Karibu kufukuza tembo, ametoa magari na pikipiki, lakini Bado havitoshi lazima tumsaidie," alisema Gungu.

Gungu alisema amefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na UWT chini ya Mwenyekiti wao na kwa upande wao watajitahidi kukaa pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii ili kuona namna bora watakavyosaidiana kukabiliana na suala la tembo kwa Wananchi wa Wilaya hiyo.

Kuhusu kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi za Chama alisema ni muhimu kila Kata kuwa na Ofisi za CCM na kwamba chama hicho kitajengwa na Wanachama wenyewe.

"Mimi leo nachangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa saruji ili Ofisi za Chama zijengwe. Nanyie muendelee jamani Chama chetu tutakijenga wenyewe,"alisema Gungu

Kuhusu bei ya Pamba Gungu alisema bei ya pamba inakwenda sambamba na bei katika soko la Dunia na kwamba Serikali imekuwa ikiwajali wakulima, Huwa inaongeza bei ili wakulima wafaidike na kilimo Chao.

Kwa upande wake Nadra Gulam aliwapa pole Wananchi wanaosumbuliwa na tembo huku akiahidi kulifikisha suala hilo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii kwa ajili ta hatua zaidi.

“ Wakazi wenzangu wa Simiyu poleni kwa changamoto ya tembo nawaahidi kuifikisha kero hii kwa kumuomba Waziri wa Maliasili na Utalii dada yangu Angela Kairuki kutafuta siku hata 2 ili aje tujadiliane nae namna nzuri ya kuwadhibiti hawa tembo wanaosumbua wakazi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi zetu. Alisema Gulam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad