HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 20, 2023

JESCA HONORE,BELLA KOMBO KUTUMBUIZA KONGAMANO LA APOSTLE ROD DENNIS

 

MSANII wa muziki wa injili Jesca Honore amewaomba Jamii kujitokeza katika kongamano la injili litakaloenda sambamba na upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza chini madaktari kutoka Texas , Marekani.

Akizungumza na Michuziblog Honore amesema kongamano hilo litahudumiwa na mhubiri wa Kimataifa na daktari Rod Dennis na jopo la madaktari wengine kutoka nchini Marekani kwa kushirikiana na madaktari wa hapa nchini.

"Kwenye mkutano huu wa nguvu ya kuinua mataifa, kutakuwa na uponyaji wa kiroho na kimwili, nitakuwa na waimbaji wengine kuwaburudisha na watu kuguswa na Mungu kwa njia ya uimbaji, kwa hiyo watu wasikose huduma hizi bure."

Kwa upande wake, mmoja wa waratibu Emanuel Ezekiel ameeleza kongamano hilo litafanyika viwanja vya TTCL Kijitonyama Dar es Salaam kuanzia Septemba 20 na 21,2023 na kuwahimiza watu wa madhehebu yote wajitokeze kwa wingi ili wapate kupima.

Mratibu wa huduma hiyo Ben Christopher kutoka Finland amewataja wasanii wengine watakaokuwepo ni Agape gospel singers, Rehema Simfukwe, Emmy Charles, Masi Masilia, John Kavishe na Harun Laston 'Zoravo'.

Mchungaji wa Kingdom of Embassy Fred Kimiti amefunguka kuwa watu wengi wamekaa wakitegemea roho wa Mungu atashuka na kuwaponya jambo ambalo sio, kwani watu wanatakiwa wapime afya zao ili kujitambua mapema na kuchukua hatua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad